Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi. (Kushoto ni Katibu Mkuu wa IPU Ndg. Martin Chungong)
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi.
Rais wa Umoja
wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu
Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei,
2024 Geneva nchini Uswisi.
Kikao hicho
kilichohusisha Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na
Kijiographia, Wawakilishi kutoka Kamati ya Uongozi, Viongozi wa Makundi ya
Wanawake na Vijana pamoja ya Uongozi wa Umoja huo kimejadili kuhusu mapendekezo
ya ajenda za Mkutano huo wa Maspika unaotarajiwa kufanyika mwakani na kuona
namna changamoto za sasa zinazoikumba Dunia zinavyoweza kuwa sehemu ya ajenda
za Mkutano huo.
Baadhi ya
changamoto zinazotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi,
ukame na njaa hususani Sub Saharan Afrika, machafuko ya amani na vita
zinazoendelea katika baadhi ya mataifa
Duniani, usawa wa kijinsia na kujenga Jumuiya jumuishi na za ushilikishwaji.
Aidha, mjadala wa demokrasia na matumizi ya akili bandia na matokeo yake nayo
ni sehemu ya ajenda zinazotarajiwa.
0 comments:
Post a Comment