Baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Mei
15,2024 kuongeza siku tano kwa vijana wenye nia na sifa za kujiunga na Jeshi la
Polisi ili kuendelea kuwasilisha maombi ya ajira idadi ya waombaji imeendelea
kuwa kubwa hivyo baadhi ya waombaji kushindwa kutuma maombi.
Jeshi la Polisi linaendelea kufanya maboresho
kwa kuandaa mazingira ya kuwezesha kupokea maombi zaidi ili kutoa fursa kwa
waombaji wote kutuma maombi yao ndani ya muda uliopangwa.
Aidha, waombaji waendelee kutuma maombi kupitia
https://ajira.tpf.go.tz/
badala ya kupitia kwenye tovuti ya Polisi www.polisi.go.tz.
0 comments:
Post a Comment