Nafasi Ya Matangazo

May 07, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika taasisi na mamlaka nchini.
 
Rais amemteua Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Doriye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
 
Aidha, Rais Samia amemteua Bw. Christopher Derek Kadio kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Bw. Kadio anachukua nafasi ya Bi. Esther Hellen Lugwisha ambaye amemaliza muda wake.
Posted by MROKI On Tuesday, May 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo