Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kulia ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard na Rajab Rajab.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Pamoja nae ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard.Mtangazaji wa kipindi Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1, Bi.Janeth Leornard akimuuliza swali Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kushito ni Rajab Rajab mtangazaji mwenza orwa kipindi hiko.
*************
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa na mambo mapya kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha wafungwa kwa upande wa Tanzania Bara na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo kwa upande wa Zanzibar na kuwaruhusu wapiga kura kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao kwa njia ya mtandao.
Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa hewani na kituo cha televisheni cha TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K amesema kuwa Tume tayari imeweka utaratibu wa kuwaandikisha wafungwa na wanafunzi hao na mfumo wa kuboresha taarifa mtandaoni upo tayari.
Kailima amefafanua kuwa utaratibu wa kuandikisha wafungwa na wanafunzi utazingatia matwaka ya sheria ambapo waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita ndio watakaoandikishwa.
Akizungumzia suala la kuanza mchakato wa uboreshaji wa Daftari mtandaoni, Bw. Kailima amesema Tume imejenga mfumo ujulikanao kama OVRS (Online Voters Registration System) utakaomwezesha mpiga kura anayeboresha taarifa zake kuanzisha mchakato mtandaoni na baadae kwenda kwenye kituo ili amalizie taratibu na kupata kadi yake ya mpiga kura.
Uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao una masharti, kwa wale ambao wanataka kurekebisha taarifa zao ni lazima wawe na namba ya NIDA, lakini, mpiga kura anayehamisha taarifa zake hatalazimika kuwa na namba ya NIDA., amesema Bw. Kailima.
Amefafanua kuwa namba ya NIDA ni muhimu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa za mpiga kura ambazo zinarekebishwa kwenye Daftari.
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amefafanua kuwa, wanaokwenda vituoni kujiandikisha kwa mara ya kwanza hawatalazimika kuwa na namba ya NIDA.
Akitoa hotuba ya kutangaza tarehe ya uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ambao unatarajiwa kufanyika mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024, Mwemyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele alisema kuwa kwa Tanzania Bara kuna vituo vya kuandikisha wapiga kura 130 vilivyopo kwenye magareza na kwa Zanzibar kuna vituo 10 vilivyopo kwenye Vyuo vya Mafunzo.
0 comments:
Post a Comment