Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2024

Balozi Maimuna Tarishi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

Amemteua Prof. Masoud Hadi Muruke kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu. Prof. Muruke anachukua nafasi ya Prof. Willy Lazaro Komba ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Bw. Ishmael Andulile Kasekwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Bw. Kasekwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili.

Amemteua Balozi Maimuna Kibenga Tarishi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Balozi Tarishi anachukua nafasi ya Prof. Joseph Rwegasira Buchweishaija ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Bw. Martin Emmanuel Kilimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara Tanzania (TCB). Bw. Kilimba anachukua nafasi ya Dkt. Edmund Bernard Mndolwa ambaye amemaliza muda wake.
Posted by MROKI On Wednesday, May 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo