Nafasi Ya Matangazo

May 13, 2024

Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt Fatuma Mganga, akizungumza na Madaktari bingwa na Bobezi 40 ambao watakuwa Singida kwa siku Saba kutoa huduma za matibabu kwa wananchi wa mkoa wa Singida.
Joachim Masunga - Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Uzazi, Mama na Mtoto akitoa maelezo kuhusu namna ya utoaji wa matibabu kwa Wananchi wa mkoa wa Singida.
Madaktari bingwa na Bobezi 40 wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida wakipokea maelekezo ya Serikali kuhusu namna ya utoaji huduma za matibabu kwa wananchi wa mkoa wa Singida.

Madaktari bingwa na Bobezi 40 wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida wakipokea maelekezo ya Serikali kuhusu namna ya utoaji huduma za matibabu kwa wananchi wa mkoa wa Singida.



Serikali ya Mkoa wa Singida imewaagiza Waganga Wakuu wa wilaya zote TANO za mkoa wa SINGIDA kuhakikisha wanapanga Wauguzi na Watalaamu wa afya kada nyingine wa kutosha ambao watashirikiana na Madaktari Bingwa na Bobezi 40 wa Rais Samia katika utoaji wa huduma mbalimbali za kiafya katika Halmashauri Saba za mkoa huo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt FATUMA MGANGA ametoa kauli hiyo wakati akiwakaribisha madaktari bingwa na bobezi wa Rais Samia ambao wamekuja mkoani Singida kusaidia matibabu ya kibingwa na bobezi kwa wananchi wa mkoa wa Singida kwa Siku Sita.

Katibu Tawala huyo amesema kazi ya utoaji wa matibabu ya kibingwa na bobezi itaenda haraka iwapo Madaktari hao wanapata wasaidizi wazuri katika kila kada kwenye maeneo ambayo watatoa huduma za afya hizo.

“Sitegemei Mwananchi yeyote wa mkoa wa Singida kukosa huduma hizi za matibabu ya kibingwa na bobezi huduma ambazo huwa wanazifuata mbali na kwa gharama kubwa hivyo wananchi wote lazima wapewe taarifa ili wapate matibabu karibu na maeneo yao,” Amesisitiza Fatma Mganga.

Amewahakikishia ushirikiano Madaktari hao Bingwa na Bobezi katika kila jambo wanalofanya lengo ni kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Singida anapata matibabu ya uhakikika kupitia wa madaktari hao Rais Samia.

Katibu Tawala pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Huduma hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa Watanzania wengi ambao baadhi yao wanashindwa kumudu gharama za kwenda kupata matibabu hayo kwenye Hospitali kubwa nchini na huduma hiyo kwa sasa wanaipata karibu na maeneo yao.

Naye, Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Uzazi, Mama na Mtoto Joachim Masunga amesema mpango huo wa kutoa matibabu ya kibingwa na bobezi utafanyika nchi nzima nia ni kuona Mtanzania anapata huduma hizo karibu na maeneo yao na kuondoa tatizo la kufuata huduma hizo mbali na kwa gharama kubwa.

Masunga amesema kwa sasa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa Hospitali na Vituo vya afya pamoja na kupeleka vifaa vya kutosha vya afya lengo likiwa ni kusaidia Watanzania kupata huduma bora na za uhakika za afya katika maeneo yao ikiwemo mpango wa kupeleka Madaktari bingwa na bobezi kwa kila wilaya ili kusaidia wananchi kupata huduma hizo kwa njia rahisi.

Posted by MROKI On Monday, May 13, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo