Nafasi Ya Matangazo

April 08, 2024






Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Manyoni kutuma timu Wataalamu Ardhi kwenda katika Kituo cha Makazi ya Wazee wasiojiweza cha Sukamahela kwa ajili ya kupima na kuweka mipaka ya kituo hicho ili kudhibiti wananchi wasivamie eneo hilo na kuanzisha shughuli za kiuchumi ikiwemo mashamba.
 
Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo leo (8-Apr-24) baada ya kutembelea Kituo hicho na kukabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo Televisheni,friji nguo, vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid.
 
Halima Dengego amesisistiza kuwa baada ya mwezi MMOJA kuisha apatiwe taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo Vinginevyo atawachukulia hatua Watendaji ambao hawatatekeleza agizo hilo nia ikiwa ni kuhakikisha Wazee wanaotunzwa kwenye kituo hicho wakaa na kuhudumiwa vizuri bila ya kubughuziwa na mtu.
 
“Hawa Wazee wametutumikia sana wametufanya tuwe hapa tulipo hivyo ni lazima tuwaheshimu,tuwalee na Tuwatunze”Alisisitiza Dengego.
 
Kuhusu Tatizo la kukosekana kwa huduma ya maji na umeme kwenye kituo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1974 kwa ajili ya kutoa huduma kwa Waathirika kwa ukoma, Mkuu wa huyo wa mkoa Singida amewataka Watendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme -TANESCO mkoa wa Singida na wa Mamlaka ya Maji waende kwenye kituo hicho na kuweka kambi ili huduma hizo muhimu ziweze kupatikana muda wote kwenye kituo hicho.
 
Mkuu huyo wa mkoa amesema siku 14 zinatosha kabisa kuweka huduma za maji na umeme kwenye kituo hicho kama hatua ya kuhakikisha wazee hao wanaishi maisha yenye staha ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.
 
Amesisitiza kuwa kupatikana kwa huduma hizo kutasaidia ulinzi kwa wazee hao pamoja na kuwaepusha na vitendo vya kushambuliwa na wanyama wakali hasa nyakati za usiku kutokana na eneo hilo kukabiliwa na vichaka vingi.
 
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Fatuma Mganga amesisitiza Watumishi wa Serikali wanaofanya kazi kwenye kituo hicho kufanya kazi kwa bidii na ufanisi katika kuwalinda na kuwatunza Wazee hao ili waishi maisha mazuri nay a furaha kama watu wengine.
 
Amesema kuwa Wazee ni hazina na baraka hivyo lazima wahudumiwe kama na kupatia huduma za msingi kama jamii nyingine.
 
Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee wasiojiweza cha Sukamahela Lusajo Kafuko ametaja changamoto mbalimbali zinazokwamisha utoaji wa huduma bora wa wazee hao ikiwemo kukosekana kwa huduma maji,umeme pamoja na kukosekana kwa mlezi wa kiume.
 
Ameeleza kuwa anaimani kubwa kuwa ujio wa viongozi hao utasaidia kutatua changamoto hizo ambazo zinakwamisha utoaji wa huduma bora kwa Wazee hao walemavu.
 
Kituo cha Makazi ya Wazee Wasiojiweza cha Sukamahela wilayani Manyoni kilianzishwa mwaka 1974 kwa ajili ya kutoa huduma za tiba kwa Waathirika wa ugonjwa wa ukoma ambapo kwa sasa kinahudumia wazee kutoka Mikoa ya Singida na Dodoma.
Posted by MROKI On Monday, April 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo