Nafasi Ya Matangazo

March 10, 2024





Na Mwandishi wetu, Dar  es Salaam
Timu ya soka ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),  TANROADS FC leo tarehe 10 Machi, 2024 imeumana na timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), TPDC FC katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanja wa TPDC Jijini Dar es Salaam.

Wenyeji TPDC wametumia vyema uwanja wao na kuibuka washindi kwa magoli 4-1 yaliyofungwa matatu na Dkt. Barnabas Mwaishamba na moja Mhandisi Buruhani, na bao pekee la TANROADS FC lilifungwa na mchezaji hodari Farid Kubanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa East Zone TANROADS, Charles Ndyetabula ambaye pia alicheza vyema  kwenye mechi  hiyo, amesema mchezo huo umewapa mafundisho mengi kutoka kwa wapinzani wao, ambapo sasa wanahitaji kuwekeza katika viwanja vya michezo.

"Tume enjoy mchezo wa leo na tumejifunza, tukiangalia TANROADS tuna maeneo mengi na sisi tunahitaji kuwekeza katika viwanja lengo kubwa la mchezo ni kufanya mazoezi, kutunza afya na kuandaa timu kwa ajili ya mashindano Mei Mosi na kufahamiana kama taasisi . Wito wangu kwa taasisi watu wajitoe na wafike tuwe wengi ili tufike mbali," amesema Ndyetabula.

Naye nahodha wa TANROADS FC, Gabriel Basel amesema amewapongeza wapinzani wao kwa kuwa pamoja  na kupata ushindi mnono na mchezo kumalizika salama.
Posted by MROKI On Sunday, March 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo