Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2024

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, akiwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Advera Mwijage kuhusu majiko yanayotumia umeme kidogo walipotembelea banda la REA kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia nje ya ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo ni Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, wakipata maelezo kuhusu mashine za kuzalisha mkaa mbadala kutoka kwa Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Mhandisi, Advera Mwijage walipotembelea banda la REA kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia nje ya ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, leo Tarehe 9 Machi, 2024.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala na Jadidifu, Mhandisi, Advera Mwijage akitoa mada kuhusu nishati safi ya kupikia kwenye Kongamano hilo katika ukumbi wa mikutano Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, leo Tarehe 9 Machi, 2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala na Jadidifu, Mhandisi, Advera Mwijage wakipata maelezo mafupi kuhusu teknolojia za nishati safi ya kupikia kutoka kwa Mdau wa Kampuni ya JIKOPOA leo Tarehe 9 Machi, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi, Hassan Saidy akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Watu waliotembelea banda la REA kwenye Kongamano hilo.
Wadau mbali mbali waliotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakipata maelezo kuhusu teknolojia mbali mbali za nishati safi ya kupikia.
************
Viongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy pamoja na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala na Jadidifu, Mhandisi, Advera Mwijage leo, Tarehe 9 Machi, 2024 wameshiriki kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia ambalo limekwenda sambamba na kuhitimisha Maadhimiho ya Siku ya Wanawake Duniani (2024) katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo ni Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliambata na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ambapo walipotembelea banda la REA ujumbe mkubwa ulikuwa ni kuendelea kutoa hamasa na elimu ya matumizi ya tekonojia rahisi na nafuu kwa Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na kurahisisha katika upatikanaji wake.

“REA kwa kushirikiana na STAMICO imefadhili ununuzi wa mashine kubwa tatu kwa ajili ya kuzalisha makaa ya mawe. Mradi huo, umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 5 na sisi kama Wakala tuna hamasisha matumizi ya mkaa mbadala (Mkaa salama) kama chanzo cha nishati safi ya kupikia”. Amekaririwa Mhandisi, Advera.

Mhandisi, Advera amemwambia, Mgeni Rasmi, Dkt. Philip Mpango kuwa REA inatekeleza jukumu la kuhakikisha nishati za aina zote zinapatikana vijijini na kwa Watu wote na kuongeza kuwa imekuwa mstali wa mbele kuwasaidia Waendelezaji wa teknolojia za nishati safi pamoja na Miradi inayolenga kwenye kuongeza upatikanaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia.

Mhandisi, Advera ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha wa 2023/2024, Wakala imetoa zaidi ya mitungi ya gesi ya kupikia 158,100 kwa Wananchi wa vijijini kama sehemu ya hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa mitungi zaidi ya laki 4 itatolewa kupitia utaratibu huo

Mhandisi, Advera ameongeza kuwa mbali ugawaji wa mitungi ya gesi, REA imeanza kutekeleza program ya kusambaza gesi asili kwa Wananchi wa vijijini wa mkoa wa Pwani na Lindi, Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 6.8 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi 980 zitaunganishwa kwenye mtandao wa gesi asilia kwenye nyumba zao.

Ameutaja Mradi mwengine ni wa kuwaunganisha Wananchi wa vijijini katika mkoa wa Pwani na Mtwara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 13.5 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi ya 1,400 zitanufaika.

Mhandisi, Advera amesema REA pia inatekeleza Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, ambapo Tanzania kuna magereza zaidi ya 129 ambapo imeelezwa kuwa matumizi ya kuni pekee yake ni zaidi ya asilimi 93. Mradi huo umeanza kutekelezwa na utagharimu shilingi bilioni 40.

Miradi mingine unaofanana na huo ni ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo kambi 26 zitanufaika na Mradi huo uliotengewa zaidi ya bilioni 3.5 ambapo utaanza kutekelezwa hivi karibu.

Mradi wa Mmwisho ambao REA imepanga kuutekeleza ni wa kujenga miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye shule kongarobaini za sekondari hapa nchi, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 2.6 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Posted by MROKI On Saturday, March 09, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo