Bashungwa amezungumza hayo
jijini Dodoma katika mkutano uliokutanisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya
Usajili ya Wahandisi (ERB), na kusisitiza kuweka mikakati mahususi ya
uendelezaji wa Wahandisi Washauri kitaaluma ili kukuza tasnia ya Uhandisi.
“Vipaumbele na maagizo ya
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
katika sekta hii ni kuona ushiriki mkubwa wa Wahandisi na Makandarasi Wazawa
katika kazi za ujenzi na usimamizi wa miradi (Local Content), sisi kama
wasaidizi wake tuhakikishe tunalitekeleza hili”, amesema Bashungwa.
Aidha, ameelekeza kuhakikisha
kunakuwa na uwepo wa ushirikishwaji wa Wahandisi wahitimu katika mpango wa
mafunzo kwa vitendo (SEAP) kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa nchini ili
kuwajengea uwezo.
Vilevile, ameagiza kuangalia
maeneo yote yenye changamoto katika Sheria ya Usajili ili kuwawezesha wahandisi
kufanya ubunifu na kusaidia nchi katika uchumi wa viwanda na maendeleo ya
Sayansi na Teknolojia.
“Tengenezeni mazingira wezeshi
kwa Wahandisi Washauri wazawa kuweza kushiriki katika miradi ili kuokoa fedha
za Serikali”, ameagiza Bashungwa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Balozi Eng. Aisha Amour, ameishauri Bodi na Manejimenti ya ERB
kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi kazini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Eng. Menye Manga, ameahidi kushirikiana
na Menejimenti ili kuleta mabadiliko chanya katika Taaluma ya kihandisi na
kuhakikisha taaluma inaendelezwa na kukuzwa ili kuongeza idadi ya wataalam hao
nchini.






.jpg)



0 comments:
Post a Comment