Shaban Lukelema Katibu Msimamizi Miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe,akizungumza na waandishi wa habari na wahariri katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoani humo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Itunduma wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe ambayeBi.Sara Mkini, akizungumza na waandishi wa habari na wahariri katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoani humo.
Mtendaji wa Kijiji cha Itunduma Bi.Tabia Mkondola akifafanua baadhi ya Mambo kwa wanahabari kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kijijini Itunduma.
****************
Shule ya Msingi Itunduma iliyoko Wilaya ya Wangin'gombe Mkoani Njombe imeondokana na changamoto ya utoro kwa wanafunzi baada ya kujengewa vyumba vitatu vya madarasa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Hayo yamebainishwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Itunduma Bi.Sara Mkini, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoani humo.
Amesema kabla ya madarasa hayo kujengwa kulikuwa na msongamano mkubwa kwenye darasa moja walikuwa wanakaa wanafunzi zaidi ya 100 hivyo kupelekea watoto kushindwa kufika shuleni kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa rafiki.
"Shule yetu inawafunzi 629 ambapo wavulana ni 320 na wasichana 309,upungufu wa vyumba vya madarasa ulikuwa ni sita kwa sasa tunaupungu wa madarasa matatu,pia tunachangamoto ya bwalo la chakula ambapo wakati wa mvua watoto wanapata shida hivyo naiomba Serikali iweze kutusaidia ili tuondokane na adha hiyo", amesema Mwalimu Mkini
Kwaupande wake Mtendaji wa Kijiji cha Itunduma Bi.Tabia Mkondola, amesema wananchi wa Kijiji hicho walijitolea nguvu kazi kwenye mradi huo ambao umeleta mabadiliko makubwa katika Shule ya msingi Itunduma.
Amesema wananchi wameupokea mradi huo kwa mikono miwili huku akieleza kuwa atashirikiana nao katika kuutunza ili uweze kuwasaidia wanafunzi kwa muda mrefu.
Shaban Lukelema ni Katibu Msimamizi Miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe, amesema kupitia mkutano wa Serikali ya Kijiji walipendekeza miradi miwili ikiwemo vyumba vya madarasa vitatu na matundu manne ya vyoo .
"Tulipata zaidi ya milioni 60 kutoka Serikali kuu na mradi ulianza rasmi mwaka jana na tulitarajia ukamilike Aprili 30, 2023 lakini kutokana na changamoto za hapa na pale ikiwemo mvua zilizosababisha barabara kuharibika hivyo kushindwa kupitisha vifaa vya ujenzi kwa wakati mradi ulikamilka Mei mwaka huu", amesema Lukelema,
0 comments:
Post a Comment