Nafasi Ya Matangazo

November 26, 2023





Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Zainabu Shomari (MNEC) amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekuwa na juhudi za kujenga na kuboresha miundombinu ya Shule mpya za Mkoa za wasichana ili kuandaa mazingira mazuri ya kujifunzia na kuongeza idadi kubwa ya  wataalamu wa jinsia ya kike wa Kada mbalimbali nchini na kuleta usawa wa kijinsia .

hayo amesemwa Leo Novemba  25, 2023 wakati alipofanya ukaguzi wa  ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Dodoma unaogharimu kiasi cha shilingi Billioni 3 iliyopo katika Kata ya Manchali Wilayani  Chamwino Mkoa wa Dodoma. 


“Rais Samia ameleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hii, uwepo wa mradi huu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Dodoma utaongeza idadi na ari ya wanafunzi wa kike kupata elimu bora.” Ameeleza Ndg. Shomari  

Akiwa katika Shule ya Wasichana Chilonwa, amewahimiza wanafunzi kuzingatia maadili kwa kuwaheshimu walimu na kusoma kwa bidii kwani wao ndio tegemeo la Taifa la kesho .

Kwa Upande Wake, Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba akijibu kero za wananchi  kuhusu  kujengewa kituo cha afya Chalinze na kuongezewa  madarasa katika Shule ya Msingi Chiburunge, amesema kwa kushirikiana na Mbunge tayari wamesha anza utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu hiyo. 

Ziara ya  UWT Taifa sasa imefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na imefanya Mikutano ya hadhara takribaini ishirini huku Makamu Mwenyekiti UWT na timu yake ikikagua ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa, Zahanati ya Manchali na ujenzi wa Mabweni matatu, Vyumba nane vya madarasa na matundu 13 ya vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Chilonwa sambamba na kugawa kadi za Wanachama wapya 100 wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Posted by MROKI On Sunday, November 26, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo