KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwalimu Abdul Maulidi amewataka wadau mbalimbali kushirikiana na serikali Ili kuhakikisha kuwa uwekezaji wa mtoto unaanza mara mama anapotunga mimba hadi mtoto kuzaliwa.
Akizungumza Katika kikao cha tathmini Cha utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) Mkoa wa Dar es Salaam, Maulidi amesema kuwa ili kujenga Taifa la baadae, mtoto anatakiwa kuanza kuwekeza angalia tumboni, mara anapozaliwa, anaendelea na uwekezaji huo hali itakayomsaidia kukua katika utimilifu wake.
Programu iliziduliwa 2021 Dodoma ambapo inalenga watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane katika afya tano za lishe, afya, elimu Jumuishi, Malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.
" Uwekezaji wenye tija unaanza mtoto akiwa tumboni, mama kuhudhuria kliniki na kupata vipimo stahiki kuanzia kwenye mimba hadi kujifungua, hivyo basi umsaidia mtoto kuwa na afya bora huku akiendelea kufuata maelezo ya watalaam wa afya na lishe mpaka atakapokua," alisema Mwalimu Maulidi.
Alisema kuwa, asilimia 90 ya ubongo wa mtoto ukua kuanzia umri sifuri hadi miaka minane, ndo kipindi ambacho Serikali, wadau na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuzingatia ili kuhakikisha mtoto anakuja Katika hali ya utimilifu wake.
" Sisi walimu tunapata changamoto ya uelewa Kwa watoto iliyosababishwa na udumavu, hata ukiwaelimisha hawaelewi, hivyo basi kila mmoja anapaswa kuwa makini katika malezi ya watoto," alisema Maulidi.
Aliongeza kuwa, Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali ili kutekeleza Programu hii ambayo ni muhimu kwa malezi.
Naye Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa huo, Nyamara Elisha alisema kuwa Programu hiyo inatekelezwa kwenye ngazi ya mkoa ambapo imegatua madaraka kwenye halmashauri, inaleta taarifa zake ili kuangalia walipofikia na wadau kujadili kwa pamoja na kuboresha kwenye maeneo yenye changamoto.
" Halmashauri zinatekeleza PJT-MMMAM kuanzia ngazi ya kata Kwa kuangalia afya tano zilizopo kwenye programu hii, kikao hiki linapitia na kujadili kwa pamoja kwenye maeneo yenye changamoto na kuziboresha ili kuhakikisha watoto wanakua katika utimilifu wake," alisema Nyamara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bright Jamii Initiative (BJI) Irene Fugara alisema kuwa, Mkoa huo umepiga hatua katika utekelezaji wa Programu hiyo ambapo kwenye eneo la afya kumekuwa na ongezeko kubwa la wazazi kuwapeleka watoto kliniki na kupata chanjo huku wakisikiliza ushauri wanaopewa na watalaam wa afya.







0 comments:
Post a Comment