Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Atupele Mwakibete (kulia) na Mshauri wa Waziri kutoka Ubalozi wa China Nchini,
Suo Peng (kushoto) wakiweka maua katika moja ya
makaburi ya Wahandisi na watendaji waliofariki katika ujenzi wa reli ya
Shirika la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), jijini Dar es Salaam.Q
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete na Mshauri wa Waziri kutoka Ubalozi wa China Nchini, Suo Peng wakiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya Wahandisi na watendaji waliofariki katika ujenzi wa reli ya Shirika la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), jijini Dar es Salaam.*************
Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema Serikali itaendelea kutenga fedha kila
mwaka kwa ajili ya kuwekeza kwenye Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
ili kuhakikisha shirika hilo linapata faida na kuweza kujiendesha.
Akizungumza
katika tukio maalum la kuwakumbuka wahandisi na watumishi mbalimbali
waliofariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo jijini Dar es Salaam Naibu Waziri
Mwakibete amesema mchango walioutoa katika ujenzi wa reli unathaminiwa hivyo
Serikali itaendelea kuutambua kwa kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa
kutimizwa kiutendaji yanafikiwa.
“Reli hii
iliasisiwa na viongozi wetu Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Dkt. Kenneth
Kaunda aliyekuwa Rais wa Zambia kwa kushirikiana na China hivyo njozi
yao ya uanzishwaji wa reli hii hatutaiacha iende hivi kwa kuangalia shirika
hili likijiendesha kwa hasara wakati wao walihakikisha shirika linakuwepo na
linakuwa na malengo ya kusafirisha mzigo na abiria kwa Tanzania na Nchi Jirani
zinazotuzunguka’ amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu Waziri
Mwakibete amesema Serikali za Tanzania na Zambia kwa kushirikiana na Serikali
ya China wako katika hatua mbalimbali za kutatua changamoto zilizopo kwa sasa
ili kuhakikisha uwekezaji unaowekwa kwa pamoja unakuwa na tija kwenye
miundombinu na mtaji.
Naye Mshauri wa
Waziri kutoka Ubalozi wa China Nchini, Suo Peng amemuhakikishia Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Atupele Mwakibete, kuwa nchi hiyo iko tayari wakati wote kuhakikisha
shirika hilo linaboreshwa kwani lilidhamiria kusaidia kwenye ujenzi hivyo
hakuna sababu ya kushindwa kulisaidia kwenye kipindi hiki cha maboresho.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching’ amesema TAZARA inatekeleza
mpango wake wa muda mrefu na mfupi ambapo kwa sasa tayari kuna kampuni ambazo zinashirikiana
nazo ili kuhakikisha uwekezaji unaoendelea kuwekwa unakuwa na faida.
Siku ya
kuwakumbuka watendaji mbalimbali walipopoteza Maisha katika ujenzi wa reli ya
TAZARA huadhimishwa aprili 1 ya kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment