Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Taarifa kutoka Ikulu inasema kuwa Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.
Aidha, katika
hatua nyingine, Rais Samia amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt.
Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro
(KADCO).
Dkt.
Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana
wa Benki Kuu.
0 comments:
Post a Comment