Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata akizungumza na waandishi wa habari, viongozi wa dini, wazee na makada wa chama hicho mkoani hapa Januari 5, 2023 wakati akitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida, William Nyalandu.
Na Dotto Mwaibale, Singida
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kinampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kukubali kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya Siasa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata akizungumza Januari 5, 2023 na waandishi wa habari, viongozi wa dini, wazee na makada wa chama hicho mkoani hapa alisema kwa hatua hiyo Rais amekuza Demokrasia nchini.
"Tunampongeza Rais kwa falsafa ya 4R ambayo imemuongoza katika kujadiliana na viongozi wa vyama vya kisiasa ili kuimarisha Umoja, Utulivu na Amani ili Serikali iendelee kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea maendeleo Wananchi" alisema Mlata.
Mlata alisema CCM Mkoa wa Singida wameona ni moyo wa kishujaa alionao Rais Samia na anastahili kupongezwa na wanaona njia hiyo aliyoitumia inakiimarisha chama hicho na kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema kitendo alichofanya Rais cha kukaa na viongozi wa vyama vyote meza moja kitawafanya na wananchi pia kuwa wamoja na kwamba ameiheshimisha nchi na jambo hilo la kuruhusu shughuli za vyama ziendelee ametimiza matakwa ya utawala bora unaoheshimu katiba.
"Tunampongeza Rais kwani ameamsha na kuchochea maendeleo kwa kuwa kwenye mikutano watu watatoa maoni yao kuhusu maendeleo ya nchi na sisi CCM Mkoa wa Singida tunakaribisha kwa mikono miwili uamuzi huo" alisema Mlata.
Alisema CCM Mkoa wa Singida wapo tayari kwa hoja za vyama vingine katika majukwaa kwa kuzingatia utekelezaji mzuri wa Ilani unaoendelea mkoani humo ambapo wanaviomba vyama vingine kutumia vizuri fursa hiyo kwa manufaa ya nchi yetu na maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
Mlata alitumia nafasi hiyo kuwaomba wana Singida kuendelee kumuombea Rais wetu, Mungu azidi kumpa afya njema, hekima, maono na umri mrefu.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa mkutano huo.
Mkutano ukiendelea. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu na kushoto ni Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Singida, Comrade Mang'olaMkutano ukiendelea.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Makada wa CCM na viongozi wa dini wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea
0 comments:
Post a Comment