Nafasi Ya Matangazo

January 04, 2025









Na: Mwandishi Wetu, Tanga.
Madereva bodaboda na bajaji Tanga Mjini kupitia Umoja wa Wamiliki na Waendesha Pikipiki na Bajaji Tanga Mjini (UWAPIBATA) wamemchangia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan fedha kiasi cha shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kuchukua fomu ili aweze kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Tukio hili la aina yake limefanyika leo Januari 04, 2025 katika viwanja vya Lamore jijini Tanga ambapo Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu alikutana na waendesha pikipiki na bajaji hao ikiwa ni jitihada zake za kuyafikia makundi yote ndani ya jimbo hilo ili kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Waendesha bodaboda na bajaji hao walionyesha kuridhika na kazi nzuri zilizofanywa na Rais Samia pamoja na Ummy Mwalimu katika Jimbo la Tanga Mjini ambazo zimegusa maisha yao kwa ujumla na kuchochea maendeleo.

Katika hatua nyingine, Ummy Mwalimu alichangia shilingi Milioni Kumi katika mfuko wa UWAPIBATA ili ziweze kuwasaidia katika mipango yao. "Bodaboda ni kazi kama kazi nyingine. Mimi kama Mbunge wa Tanga Mjini, nitaendelea kuwathamini na kushirikiana nao ili kuboresha mazingira ya kazi zao. 

"Kipekee nimevutiwa mno na kitendo cha madereva bodaboda na bajaji Tanga Mjini kumchangia pesa Rais wetu mpendwa Dk. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuchukua fomu ya Urais". 

"Kiukweli Rais Samia amefanya kazi kubwa sana Tanga Mjini ikiwemo maboresho ya Bandari ya Tanga ambayo yameongeza fursa za biashara kwa madereva bodaboda na bajaji." amesema Ummy Mwalimu.
Posted by MROKI On Saturday, January 04, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo