Nafasi Ya Matangazo

November 02, 2022

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akijibu maswali ya wabunge Bungeni  Novemba 2,2022 wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa tisa wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.

Serikali imesema haioni haja ya kupunguza eneo la hifadhi ya msitu wa Mbiwe ili litumike kwa matumizi ya Wananchi na shughuli za Kiuchumi.
 
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) , alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Njelu aliyetaka kujua endapo Serikali inaona haja ya kupunguza eneo la hifadhi ya msitu huo kwa wananchi.
 
“Lengo la kuanzishwa hifadhi hiyo ni kulinda bioanuai zilizomo ndani ya hifadhi ikiwemo; vyanzo vya maji vinavyotumika kwa matumizi ya binadamu na wanyamapori,”alisema Naibu Waziri Masanja.
 
Aidha Masanja amesema, Sheria ya misitu inaruhusu uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo kwa njia endelevu.
 
Hifadhi ya Msitu wa Mbiwe ipo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Posted by MROKI On Wednesday, November 02, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo