Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2024








Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imelielekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) kuongeza uwezeshaji kwa wananchi ili waweze kuhamasika kutumia mfumo wa gesi kwenye magari yao kwani una gharama nafuu  na utaokoa fedha za kigeni zinazotumiwa na Serikali kuagiza mafuta nje ya nchi.

Mwenyekiti hiyo, Mhe. Dkt. Mathayo  David Mathayo alisema hayo wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kupitia TPDC  ya kuwaelimisha Wabunge juu ya mkakati wa TPDC kwenye utekelezaji wa miradi yake ya kimkakati kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

‘’ Wananchi wanahitaji sana huduma ya gesi kwenye magari yao lakini upatikanaji wa vituo vya kujaza gesi ndio hofu yangu, nashauri mjipange kuhakikisha kila Mkoa angalau unakuwa na vituo ili kusogeza huduma karibu na wananchi.’’Alisema Mhe. Dkt. Mathayo.

Alieleza kuwa, Tanzania inayo hazina kubwa ya gesi hivyo ni vema kutumia fursa hiyo kwa kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa TPDC ione umuhinu wa kusogeza karakana za kuweka mifumo ya CNG  kwenye magari kwenye maeneo mengine, badala ya kutegemea Dar es salaam pekee jambo ambapo ni usumbufu na gharama kuifuata huduma huko.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema, Wizara ya Nishati itaendelea kuiwezesha TPDC kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa miradi hii inakuwa na tija na kukamilika kwa wakati na ndio maana wamehusisha sekta binafsi kushiriki kwenye ujenzi wa vituo vya  CNG na kuwezesha karakana za kuweka mifumo ya CNG kwenye Magari .

Katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 TPDC inejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya utafutaji wa gesi na uendelezaji wa mafuta, miradi ya usafirishaji na usambazaji wa gesi,miradi ya kutekeleza mkakati wa Nishati safi ya kupikia.

Posted by MROKI On Friday, June 28, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo