Nafasi Ya Matangazo

November 02, 2022

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akijibu maswali ya wabunge Bungeni  Novemba 1,2022 wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa tisa wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.
***********
SERIKALI imesema inaendelea kuchukua jitihada za kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji katika maeneo mbalimbali nchini hususan katika Jimbo la Kibaha Vijijini.  
 
Hayo yamesema Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Costantino Mwakamo aliyetaka kujua Serikali imejipanga vipi kutatua migogoro ya ardhi ya muda mrefu kati ya wananchi na wawekezaji wenye mashamba makubwa Kibaha Vijijini.

Kikwete akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kufanya ukaguzi wa ardhi iliyomilikishwa kwa wawekezaji ili kubaini iwapo masharti ya umiliki yanazingatiwa.
 
Pia alisema Serikali inachukua hatua za ubatilisho kwa wawekezaji waliobainika kukiuka masharti ya umiliki; kupanga upya ardhi iliyobatilishwa kwa kushirikiana na Mamlaka za Upangaji kulingana na mahitaji halisi ya sasa hususan hazina ya ardhi, huduma za kijamii na makazi.
 
Aidha, Wizara inaendelea kutoa elimu kwa jamii na wawekezaji kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria na miongozo ya sekta ya ardhi ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Aidha katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kiwete amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mch. Joseph Gwajima kufuatilia na kutatua changamoto zilizopo katika eneo la Chasimba.

Posted by MROKI On Wednesday, November 02, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo