Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (kulia) amemkabidhi Waziri wa Utalii na Maliasili Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Wananchi wa kaya 23 zenye watu wapatao 113, Hati ya Makazi na Mashamba 23 , Vitalu 6 vya Malisho vyenye ukubwa wa Hekta Elfu 22, maeneo ya Viwanja na mashamba yaliyopimwa 5,230 yaliyokwishapima 14,579 wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wananchi wapya wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga Tarehe 16 Juni 2022 katika kijiji cha Msomera mpakani Mwa Wilaya ya Handeni na Kilindi, Mkoa Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kimila wa kabila la Maasai walilokuwa wakiishi katika Hifadhi ya Ngorogoro, Laigwanani Matigoi Tauwo.
Mkuu wa Kimila wa kabila la Maasai walilokuwa wakiishi katika Hifadhi ya Ngorogoro, Laigwanani Matigoi Tauwo akizungumza na kumshukuru Mungu kwa kumuongoza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Sulauhu Hassan kwa maono yake ya kuwapatia Makazi Bora katika Kijiji Cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Tanga.
wakazi hao wapya wa Handeni
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndg. Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati wa kukabidhi hati kwa hati hizo.
Mkuu wa Kimila wa kabila la Maasai walilokuwa wakiishi katika Hifadhi ya Ngorogoro, Laigwanani Matigoi Tauwo akionesha hati hizo baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt Pindi Chana.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nummba na Maendeleo ya Makazi, Ridhwani Kikwete akisalimiana na wananchi hao wapya wa Handeni.
Mkuu wa Kimila wa kabila la Maasai walilokuwa
wakiishi katika Hifadhi ya Ngorogoro, Laigwanani Matigoi Tauwo amemshukuru
Mungu kwa kumuongoza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa maono yake ya kuwapatia Makazi Bora katika Kijiji Cha Msomera
kilichopo Wilaya ya Handeni Tanga.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wenzake wa
Ngorogoro ambao wameamua kuhama kwa hiyari yao, Laigwanani Tauwo amesema sasa
maisha yao yatakuwa ya amani zaidi na yenye maendeleo kuliko huko nyuma kwa
kuwa Serikali imewapatia Nyumba, Ardhi kwa ajili ya Killimo na Ufugaji, pia
huduma bora za kijamii kama elimu na afya.
“Namshukuru sana Mungu kwa kutupa Rais Mama
Samia, leo sisi tunamiliki nyumba jamani, kweli Mungu mkubwa sana, tunaahidi
tutaishi vizuri sana na ndugu zetu wa hapa msomera” amesema Laigwanani Tauwo.
Katika zoezi la kuwapokea wananchi hao
walioamua kuhamia Kijiji Cha Msomera ili kupisha shughuli za uhifadhi
Ngorongoro, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana
amewakabidhi wananchi hao hati za Ardhi zilizotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi.











0 comments:
Post a Comment