
Mwonekano wa nyumba zinazoendelea kujengwa na Watumishi Housing Investiment (WHI) eneo la Kisasa Njedengwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment, Dkt. Fred Msemwa (Wa kwanza kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba eneo la Kisasa Njedengwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akiangalia ramani inayoonyesha mradi wa ujenzi wa nyumba eneo la Kisasa Njedengwa zinazojengwa na Watumishi Housing Investiment (WHI) alipofanya ziara yake ya kikazi jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (Wapili kutoka kulia) akielekea kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba zinazoendelea kujengwa na Watumishi Housing Investiment (WHI) wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment, Dkt. Fred Msemwa.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Watumishi Housing Investiment (WHI) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) kabla ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba zinazoendelea kujengwa eneo la Kisasa Njedengwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment, Dkt. Fred Msemwa akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (Wapili kutoka kushoto) kwa kufanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba zilizopo eneo la Kisasa Njedengwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na watumishi wa Watumishi Housing Investiment (WHI) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba zinazoendelea kujengwa eneo la Kisasa Njedengwa jijini Dodoma.
*************
Na James Mwanamyoto,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema
Watumishi Housing Investment (WHI) inajenga nyumba bora za gharama nafuu kwa
ajili ya kuwakopesha na kuwauzia watumishi wa umma, ikiwa ni utekelezaji wa kipaumbele
cha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan cha kutatua changamoto ya makazi kwa
watumishi wa umma nchini.
Waziri Jenista amesema malengo na maono ya Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa makazi bora kwa watumishi wa umma nchini,
yanakuwa ni kipaumbele kimojawapo katika Serikali ya Awamu ya Sita
anayoiongoza.
“Bajeti kuu ya Serikali inayojadiliwa
hivi sasa inajumuisha bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora ambayo katika vipaumbele ilivyoviweka ni kuiwezesha Watumishi
Housing kupunguza changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma wote nchini,” Mhe.
Jenista amefafanua.
Mhe. Jenista amesema kuwa, eneo
ambalo Watumishi Housing Investment (WHI) inatakiwa kulifanyia kazi katika
mwaka wa fedha 2022/2023 ni kuelekea kwenye halmashauri na wilaya mpya ili
kuanza ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu ambazo zitauzwa au kukopeshwa
kwa watumishi au halmashauri kwa utaratibu unaotumiwa na WHI lengo likiwa ni
kuhakikisha watumishi wa umma nchini wanapata makazi bora.
Akizungumzia ununuzi wa nyumba
zilizojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma, Mhe Jenista amesema ni nyumba
bora na jambo la kufurahisha ni kwamba, kwa asilimia zaidi ya 95 zimenunuliwa
na watumishi wa umma.
Ameongeza kuwa, nyumba zilizouzwa
zipo za madaraja mbalimbali kulingana na uwezo wa watumishi.
“Jambo la msingi ninalopenda
kuendelea kuwasisitiza Watumishi Haousing Investment ni kujenga nyumba zenye gharama
nafuu ambazo watumishi wa ngazi ya chini wanaweza kumudu na ikiwezekana
zijengwe ambazo zitakuwa na bei ya chini zaidi ya milioni 45”, Mhe. Jenista
amesisitiza.
Akizungumzia ujenzi wa nyumba katika
eneo la Njedengwa jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing
Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa amesema mradi huo wa nyumba unaotekelezwa na
taasisi yake unahusu ujenzi wa nyumba 133 ambapo nyumba 90 zimeshakamilika na
walengwa walishahamia na nyingine 43 ujenzi bado unaendelea.
Serikali ya
Awamu ya Sita kupitia Watumishi Housing Investment (WHI) ina lengo la kujenga
nyumba bora za gharama nafuu kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma na
wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuwawezesha kupata makazi bora yatakayowawezesha
kuwa na ari na morali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.










0 comments:
Post a Comment