Nafasi Ya Matangazo

June 29, 2022

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba ,akizungumza  wakati wa kupokea gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB hafla iliyofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba ,akisisitiza jambo  wakati wa kupokea gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB hafla iliyofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vina na Walemavu, Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea  gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB  leo Juni 29,2022 jijini Dodoma hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea  gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB  leo Juni 29,2022 jijini Dodoma hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
Naibu Katibu Mkuu Wizara  Fedha na Mipango Bw. Lawrance Mafuru ,akizungumza  wakati wa kupokea gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB hafla iliyofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,akielezea kuwa  gawio hilo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 268.2 baada ya kodi ambayo Benki hiyo imeipata katika mwaka wa fedha 2021,wakati wa kukabidhi gawio la Serikali lililotolewa na benki hiyo l leo Juni 29,2022 jijini Dodoma hafla iliyohudhuriwa  na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa,akizungumza wakati wa kukabidhi gawio la shilingi bilioni 36 kwa Serikali lililotolewa na Benki ya CRDB hafla iliyofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba,akipokea Mfano wa Hundi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,wakati wa hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi  gawio la shilingi bilioni 36 kwa Serikali leo Juni 29,2022 jijini Dodoma  hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba,akimkabidhi Mfano wa Hundi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vina na Walemavu, Mheshimiwa Patrobas Katambi ambaye alipokea gawio kutokana na uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,wakati wa hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi  gawio la shilingi bilioni 36 kwa Serikali leo Juni 29,2022 jijini Dodoma  hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRD.OTMI9966
OTMI9669
OTMI9681
OTMI9477
OTMI9517
OTMI9687

OTMI0017
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba ,ak itiwa katika picha ya pamoja mara baada ya upokea gawio la shilingi bilioni 36 kutoka Benki ya CRDB hafla iliyofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRRDB.
********
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amepokea gawio la shilingi bilioni 36 linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya Benki ya CRDB kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay.

Makabidhiano hayo ya hundi kifani yamefanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma  na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi na mashirika ya umma yenye hisa ndani ya Benki ya CRDB na Menejementi ya Benki ya CRDB.

Akizungumza katika hafla hiyo Wazir wa Fedha ameipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, Dkt. Nchemba aliipongeza Benki ya CRDB kwa kupata matokeo mazuri ya fedha mwaka 2021 ambayo yamepelekea kuongezeka kwa gawio kwa wanahisa ikiwamo Serikali.

“Ongezeko hili la gawio ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki yetu ya CRDB inazidi kuimarika zaidi kutokana na mikakati madhubuti ya kibiashara iliyojiwekea na jambo linalowapa moyo Watanzania na wawekezaji kuwa benki inatoa huduma bora katika jamii, amesema Dkt. Nchemba. 

Dkt. Nchemba amesema kuwa fedha zilizopatikana kupitia gawio hilo zitakwenda kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo Serikali imeianisha katika vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2022/2023. "Kipekee kabisa niipongeze Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Benki ya CRDB kwa kazi nzuri mnayoifanya," ameongeza Dkt. Nchemba. 

Ameipongeza Benki ya CRDB kwa matokeo mazuri ya fedha iliyopata katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2020 ambapo faida ya Benki imeongezeka kwa asilimia 111 kufikia shilingi bilioni 90 kutoka shilingi bilioni 43 zilizoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2021. Mkiendelea na kasi hii mwakani tunategemea kupata gawio nono zaidi, alisema Dkt. Nchemba.

Aidha Dkt. Nchemba amezitaka taasisi nyengine kuiga mfano wa Benki ya CRDB katika kuleta faida kwa Serikali na Wanahisa kutokana na Uwekezaji. Alizitaka Taasisi na Mashirika yote ambayo Serikali inahisa kuweka mikakati madhubuti itakayoleta tija, huku akiwataka viongozi wake kutjitathmini kiutendaji.

Akizungumzia umuhimu wa ushiriki wa taasisi za fedha katika maendeleo ya taifa, Dkt. Nchemba ameipongeza Benki ya CRDB kwa kupunguza riba katika mikopo ya kilimo na wafanyakazi. Kiwango cha riba cha tarakimu moja katika mikopo ya kilimo kufikia asilimia 9 kutoka asilimia 20 iliyokuwa ikitozwa hapo awali ni cha kihistoria, hongereni sana, alisema.

Aidha, aliipongeza Benki kwa kutenga fedha kwa ajili ya uwezeshaji kwa kundi la wajasiriamali nchini kwa ajili ya kuwasaidia kuondokana na changamoto zilizotokana na janga la UVIKO-19. Kwa upande wa sekta ya kilimo alibainisha mkataba ambao benki hiyo imeingia na Shirika la Umoja wa Mataifa la GCF kuwezesha kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi utasaidia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hiyo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 268.2 baada ya kodi ambayo Benki hiyo imeipata katika mwaka wa fedha 2021. Pia ameeleza kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi kwa ujumla.

Katika Mkutano wa Wanahisa uliofanyika kidijitali mwezi Juni mwaka huu, Wanahisa wa Benki ya CRDB walipitisha kwa pamoja gawio la shilingi 36 kwa hisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 64 na hivyo kufanya gawio la mwaka huu kufikia shilingi bilioni 94, aliongezea Nsekela. Nsekela amemhakikishia Dkt. Nchemba kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya Tupo Tayari itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini huku akielezea kuwa benki hiyo sasa hivi imejikita zaidi kwenye uwekezaji wa mifumo ya kidijitali ya kutolea huduma kama CRDB Wakala, SimBanking, na Internet banking kurahisisha upatikanaji wa huduma. Pamoja na kukabidhi gawio kwa Serikali kuu kupitia mfuko wa uwekezaji wa DANIDA, Benki ya CRDB pia imekabidhi gawio kwa taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwamo PSSSF, NSSF, ZSSF, NHIF, Local Government Loans Board, Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU), Umoja Unit Trust Scheme, pamoja na halmashauri Mbinga, Shinyanga, Mufindi, Chunya na Rungwe.

Akipokea gawio kutokana na uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vina na Walemavu, Mheshimiwa Patrobas Katambi,amehimiza taasisi nyegine za umma nchini kuwekeza katika hisa ili kupanua wigo wa mapato katika taasisi zao. Serikali ndio mwanahisa mkubwa ndani ya Benki ya CRDB kutokana na kuwa na umiliki wa asilimia 21 kupitia mfuko wa uwekezaji wa DANIDA kushirikiana na Serikali ya Denmark, huku taasisi na mashirika ya umma yakiwa na umiliki wa hisa za asilimia 17.1.

Posted by MROKI On Wednesday, June 29, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo