Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye akiwa na wataalamu na viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati
wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za
Makazi
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikagua miundombinu ya Anwani za Makazi katika Mkoa
wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya
Anwani za Makazi mkoani humo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima wakati
wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za
Makazi katika Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima wakati wa
ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi
kwenye barabara, mitaa na nyumba mbalimbali katika Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa
utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi kwenye barabara, mitaa na nyumba
mbalimbali katika Mkoa wa Tanga. Katikati mwenye kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Mhe. Adam Malima.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi
(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakifurahia jambo baada ya kumaliza
ziara ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika
Mkoa huo.
*************
Waziri wa Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemuelekeza Mkuu wa Mkoa
wa Tanga, Adam Malima kuhakikisha anawachukulia hatua wale watakaobainika
kukwamisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika Mkoa huo
Akizungumza leo
Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2022 jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua
mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Waziri Nape
ameonesha kutokuridhishwa na kasi ya utekelezaji katika Mkoa huo unaoshika
nafasi ya pili kutoka mwisho
“Hili la Operesheni
ya Anwani za Makazi ni jambo letu sote, tuone shida ya kuwa mkiani, wanaotukwamisha
washughulikiwe na kama kuna shida kwenye utekelezaji tuelezane tutatue kwa
pamoja”, Amezungumza Waziri huyo
Waziri Nape
amesisitiza kuwa uwekaji wa Anwani za Makazi sio zoezi la kawaida ni operesheni
maalum iliyotangazwa na Rais, ambapo kukamilika kwake kutarahisisha kufanyika
kwa sensa ya watu na makazi na ufikishaji wa huduma mbalimbali za kijamii na
kiuchumi
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima amekiri utekelezaji wa Operesheni hiyo bado
haujaanza katika halmashauri tatu za Mkoa huo, ambazo ni halmashauri ya Korogwe mji, Korogwe vijijini na
Kilindi kutokana
na changamoto za kiutendaji
Kwa
upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.
Jim Yonazi amesema kuwa Mfumo wa kielektoniki unaoingiza taarifa za wakazi na
makazi unafanya kazi vizuri, na Wizara hiyo ipo tayari kutoa wataalamu kwenda
kuongeza nguvu kwenye mkoa au halmashauri yeyote ambayo ina uhitaji.
0 comments:
Post a Comment