Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa
utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi kwenye barabara, mitaa na nyumba
mbalimbali katika Mkoa wa Tanga. Katikati mwenye kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Mhe. Adam Malima.
*********
Waziri wa
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nauye amezikumbusha
taasisi za TANROAD na TARURA kuweka majina ya barabara ili kurahisisha Operesheni
ya Anwani za Makazi
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni hiyo Mkoani
Kilimanjaro, Waziri Nape amesisitiza kuwa iko hatari ya ukiritimba unaoweza
kufanywa na baadhi ya watu kwa kujiita majina ya mitaa yote na barabara kwa
kigezo cha kuchangia fedha za utekelezaji wa zoezi la uwekeji wa Anwani za
Makazi.
"Haya ni maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu kwamba
TANROAD na TARURA kwasababu barabara zote ni za kwao wahakikishe wanaweka
majina ya hizi barabara ili isaidie kasi ya kukamilisha zoezi hili na mie naomba
niwakumbushe watekeleze maelekezo kwa kuweka majina ya hizi barabara ili kuzipunguzia
mzigo halmashauri na kuongeza kasi ya utekelezaji wa operesheni ." Amesema Waziri
huyo
Ameongeza
kuwa, viongozi na wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kuweka majina ya mitaa
kwa kuwa kuna wadau wanajitolea, wanachangia fedha zao lakini ni vizuri majina
yawe yenye uzalendo na yanayoendana na uhalisia wa nchi yetu yakiwemo majina ya
viongozi pamoja na watu mashuhuri.
Katika hatua nyingine, Waziri Nape ameonesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa operesheni
hiyo katika
Mkoa wa Kilimanjaro ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 99.1.
0 comments:
Post a Comment