Waziri wa Maliasili na Utalii,
Balozi Dkt. Pindi Chana amewasihi Watanzania wajitokeze kwa wingi katika
maadhimisho ya kusherehekea miaka 100 ya Urithi wa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere yatakayofanyika Aprili 13, 2022 Butiama mkoani Mara ambapo mgeni rasmi
atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa.
Akizungumza leo Jijini Dodoma
Balozi Dkt. Chana amesema lengo la maadhimisho hayo ambayo yanafanywa na Wizara
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na mkoa wa Mara ni kuenzi na kusherekea mchango maridhawa
alioutoa Hayati Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere katika Nyanja mbalimbali kitaifa na Kimataifa
Waziri Chana ameeleza kuwa
maadhimisho hayo ni moja ya sehemu ya kutekeleza mpango wa Miaka 10 wa kuenzi
Urithi wa maisha ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere ambao unalenga kuwashirikisha wadau ili kujenga
uelewa wa pamoja kuhusu mchango wake na umuhimu wa kumuenzi Mwalimu Nyerere ,
kukusanya, kuendeleza, kuhifadhi na kutangaza rasilimali za urithi wa Mwalimu
Nyerere kwa manufaa ya kiazi cha sasa na kijacho ili kukuza na kuedeleza
utalii.
“Tarehe 13 Aprili, 1922 ndiyo
siku aliyozaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kama angekuwa hai tarehe
13 Aprili, 2022 angetimiza miaka 100, hivyo tunasherehekea kuenzi Urithi wa
maisha ya Hayati Baba wa Taifa ” amesisitiza
Balozi Dkt. Chana
Waziri Chana amewaalika
wananchi na wadau mbalimbali wakiwemo
waandishi wa habari kushiriki kikamilifu
katika maadhimisho hayo ya kumuenzi
Baba wa Taifa Mwl. Julius
kambarage Nyerere ambapo maandalizi ya maadhimisho hayo yanafanywa na Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Mara.
“Wizara ya Maliasili na Utalii
kwa kushirikiana na Mkoa wa Mara tunawaalika wananchi na wadau wote kushiriki kwenye kilele cha maadhimisho haya
vilevile kuendelea kuenzi kwa vitendo Urithi wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere Baba wa Taifa letu”
Aidha,amesema kuwa kuelekea
kilele cha maadhimisho hayo matukio mbalimbali yanaendelea kufanyika ikiwa ni
pamoja na mikutano ya wadau mbalimbali, mashindano ya baiskeli, matembezi ya
hiari na midahalo inayoendeshwa na taasisi mbalimbali.
Pa amesema wakati wa kilele
cha maadhimisho hayo kutakuwa na burudani mbalimbali,programu za wanafunzi za
kielimu, uzinduzi wa Mpango wa kuenzi Urithi wa Mwalimu Nyerere,nembo maalum ya
Mwalimu@100 pamoja na onesho maalum la Mwalimu Nyerere.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




0 comments:
Post a Comment