BONDIA Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ ametamba kumgalagaza kwa kichapo kitakatifu mpinzani wake Nasibu Ramadhani.
Mabondia hao watakutana na katika mpambano wao wa raundi 10 uliopangwa kufanyika Septemba 24,2021 utakao fanyika jijini Dar es Salaam.
"Nasibu amekuwa na maneno sana, hivyo nataka nimkate ngebe kwa kumpiga K.O mbaya sana ambayo aijawai kutokea katika maisha ya ngumi kwani ndio itakuwa mwisho wake wa kucheza mchezo wa masumbwi nchini, ," alisema Class.
Class ameomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kuangalia mpambano huo ambao amepania kucheza mchezo mzuri ambao utawafurahisha na kuwaburudisha wapenzi wa mchezo huo.
Nae bondia Nassibu Ramadhani alijibu mapigo kwa kusema kuwa kwa sasa Class hata mpa upenyo na kusema kuwa mpambano wao wa awali ulipoteza kwa sababu mbalimbali.
"Pambano la mara ya kwanza alibebwa, hivyo kwa sasa nimemuandalia kipigo kitakatifu ambacho ato kisahau maishani mwake, mimi huwa kwangu ni vitendo tu sina mambo mengi katika mchezo wa ngumi na sina muda wa kuongea ongea kumaliza maneno na kubwabwaja hovyo," alisema Ramadhani.
Promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ kutoka katika kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion amesema wamejipanga kuwaletea mapambano yenye tija kwa mabondia na yenye upinzani mkubwa ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi wapate burudani.
Mhamila alisema siku hiyo kutakua na mapambano saba na mabondia wote wameshasaini mkataba.
Amewataja mabondia watakao pigana siku hiyo mbali na Class na Ramadhani kuwa ni pamoja na Juma Choki atakaezipiga na Issa Nampepeche,Vicent Mbalinyi atakaezipiga na Shedrack Ignas wakati Waziri Rosta atazipiga na Anuary Mlawa.
Mabondia wengine watakao panda jukwaani ni Albano Clement atakaezipiga na Ramadhani Migwede, Daudi Mwita atakuwa akizipiga na Saidi Ndilimo
Aidha mabondia wanawake nao watapanda jukwaani kuoneshana umwamba ambapo katika pambano hilo la raundi sita litawakutanisha Agnes Kayange atakayezipiga na Lulu Kayage.







0 comments:
Post a Comment