Nafasi Ya Matangazo

July 18, 2026



📍Bagamoyo - PWANI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kusimamia sheria za Forodha kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo ushindani wa haki katika biashara na kulinda mapato ya Serikali.

Katika operesheni iliyofanyika tarehe 16 Julai 2026 wilayani Bagamoyo, TRA imekamata Jahazi likiwa na katoni 50 za sabuni aina ya Malaika Brown Soap, zilizoingizwa nchini kinyume na taratibu za Forodha. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria unaolenga kuimarisha biashara halali.

TRA Mkoa wa Pwani inaendelea kuwahimiza wafanyabiashara kuzingatia sheria na taratibu za Forodha, huku ikiahidi kuendelea kutoa huduma kwa weledi, kulinda ushindani wa haki na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Posted by MROKI On Saturday, July 18, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo