Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini'
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Msanii Mkongwe wa Taarab Asilia Nchini Bibi Mariam Hamdani, alipokutana nae katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, kabla ya kuanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, wakati wa kuanza kurekodi rasmi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,202. PICHA NA IKULU.
*********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, ameanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya
kuratibu Mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, amesema Mhe. Rais Samia
atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji,
sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.
Mhe. Rais Samia na wageni hao wa Royal Tour wameanza zoezi hilo la
kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji tarehe 28 Agosti,
2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.








0 comments:
Post a Comment