************
BENKI ya , TPB, imekabidhi vyoo vyenye matundu 20 kwa shule ya msingi Ifwagi Halmashauri ya Mufundi mkoani Iringa Julai 05 Mwaka huu .
Akizungumza wakati wa kukabidhi Majengo hayo Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Benki ya TPB amesema TPB msaada huo ni sehemu ya TPB kurudisha faida kwenye jamii kutokana na kuiunga mkono benki hiyo.
Myonga amesema kuwa richa ya kuikabidhi majengo hayo pia benki hiyo itatoa samani za ofisi za walimu ambazo waliomba shule kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi shuleni hapo
aidha ametaja baadhi ya maeneo ambayo TPB wamekuwa wakitoa msaada kuwa ni pamoja na sekta ya afya kwa kutoa vifaa tiba, mashuka magodoro na sekta ya elimu ambapo husaidia kutoa madawati, viti, meza na kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya shule na vituo vya afya.
Pia ametoa rai kwa wanafunzi pamoja na walimu kuwa wayatunze majengo hayo ili yaweza kukaa kwa muda mrefu na kusaidia watoto wengine huko mbeleni sanjali na kuwataka wananchi wote wa kijiji cha Ifwagi kukaribia katika tawi la TPB lililopo Mafinga mjini kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kibenki kwa gharama nafuu.
Akipokea Msaada wa Majengo hayo Mwalimu wa shule hiyo, Bi Imani Nyoni amesema kwa muda mrefu walikuwa wakijaribu kuomba wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya wanafunzi pamoja na walimu pasipokupata mafanikio hivyo kukabidhiwa majengo hayo na Tpb ni faraja kubwa kwao..
Amesema Shule hiyo ya Ifwagi ina jumla ya wananfunzi 211 ambao ni idadi kubwa ya wanafunzi na kulikuwa na uhaba wa matundu ya vyoo hali ambayo ilipelekea baadhi ya wananfunzi kujisaidia nje ya shule hiyo ameishukuru Tpb kwa kuondoa changamoto hiyo.
0 comments:
Post a Comment