Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007)
Mroki Mroki-Father Kidevu
Sekunde, Dakika, Saa, Siku,
Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika 13 sasa imetimia tangu Mzee Shauri
Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama
ulivyotutangulia kuja duniani.
Nimajonzi sana kwetu hasa
ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki
'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.
Unakumbukwa na wengi sana
maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O
Nathan pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.
Wananchi na majirani zako wa
pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani
Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko
yako.
Tunakumbuka maneno yako ya
Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba
hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo
daima.
Tunazidi kukuombea Baraka na
pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa
duniani.
Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.
0 comments:
Post a Comment