Mwandishi wetu.Serengeti
Arusha.Sekta ya Utalii nchini, inatarajiwa kuimarika zaidi kutokana na uwekezaji wa zaidi ya sh 6 bilioni katika ujenzi wa hoteli za kitalii na kambi tatu za kitalii za wageni maarufu eneo la Serengeti na pori la akiba la Maswa ili kukuza sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwiba Holdings na Friedkin Group,Jean Claude, akizungmza katika uzinduzi kambi ya kitalii ya Mila,ambayo inatarajiwa kuanza kupokea watalii katika eneo la serengeti na kupunguza tatizo la vitanda kwa watalii amesema ni faraja kubwa kwao kuendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya utalii nchini .
Amesema uzinduzi wa kambi hiyo, utafatiwa na kambi nyingine mbili za kitalii ambazo zitakuwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Serengeti pia na pori la akiba la Maswa ambapo, kampuni hiyo imewekeza.
Claude alisema Mwiba holdings hadi sasa imewekeza kiasi cha dola 3 na tayari imetoa ajira kwa watu 120 katika maeneo iliyowekeza kaskazini mwa hifadhi ya Serengeti na eneo la pori la akiba la Maswa.
Alisema kuanzishwa kambi hizo za kitalii,ikiwa pia ni mkakati wa kuendeleza uhifadhi na utalii endelevu wa taasisi ya friedkin Conservation Fund(FCF) katika eneo la ikolojia ya serengeti na maeneo mengine nchini.
amesema ujenzi wa kambi, kutaongeza vitanda 50 vya watalii lakini pia mchango wa kampuni hizo katika sekta ya Utalii utaongezeka zaidi.
Amesema ujenzi wa kambi hizi kutaongeza vivutio vya watalii hasa kutokana na huduma nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa kutalii kwa kutumia chopa kuona wanyama mbali mbali katika ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania.
Alisema uwekezaji wa kampuni zilizochini ya friedkin utaendelea kuwa na faida na manufaa makubwa kwa watanzania wote kwa kuzingatia uadilifu na hivyo kiunua sekta ya utalii nchini.
Kampuni za Friedkin zimewekeza maeneo mbali mbali nchini, katika utalii wa picha, uwindaji wa kitalii na masuala ya uhifadhi wa mazingira,wanyamapori na kutoa misaada mbali mbali za kijamii.
0 comments:
Post a Comment