Nafasi Ya Matangazo

January 19, 2020

 Mkuu wa wilaya Frank Mwaisumbe akitangaza kuondolewa rasmi kampuni ya Green Miles safari ltd.

Na Mwandishi wetu,Longido
Kampuni ya Green Miles iliyokuwa inamiliki kitalu cha uwindaji cha Lake Natron (East) wilaya ya Longido mkoani Arusha imetakiwa kuondoka Katika kitalu hicho ifikapo jumatatu January 20.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mundarara,Mkuu wa wilaya Longido, Frank Mwaisumbe kampuni inatakiwa kukabidhi serikali kitalu hicho kwa amani.

Mwaisumbe alisema kampuni hiyo,baada ya kutakiwa kuondoka katika kitalu hicho na serikali mwaka Jana iliomba kuongezewa muda hadi desemba 16 ili ikamilishe uwindaji na kukubaliwa na wizara ya maliasili na utalii.
Alisema baada ya kuongezwa muda kampuni hiyo, imeendelea kuwepo na sasa serikali imetoa barua nyingine kupitia katibu mkuu wizara ya maliasili na Utalii profesa Adolf Mkenda ambayo inataka mwekezaji kuondoka ifikapo jumatatu January 20.

Diwani wa Kata ya Mundarara,Alais Mushao  Longido wanaipongeza serikali kwa kumuondoa mwekezaji huyo.

Mushao alisema mwekezaji huyo alikuwa hana mahusiano na vijiji,madiwani na serikali tangu aanze uwindaji mwaka 2013 hajalipa malimbikizo ya tuzo sh350 milioni.

Mkazi mwingine wa kijiji cha Mundarara, Julius Malulu alisema kampuni hiyo imekuwa haina mahusiano na vijiji ikiwepo kushindwa kulipa tozo mbalimbali.
Michael Laizer aliyekuwa mbunge wa Longido,alimpongeza Rais John Magufuli Kwa uamuzi wa kuiondoa kampuni hiyo.

"Tunampongeza Rais Magufuli,Wizara ya Maliasili na Utalii. mkuu wa mkoa Arusha na Mkuu wa wilaya Kwa uamuzi huu wa kuiondoa kampuni hii ambayo imekuwa kero Kwa Wananchi"alisema.

Waziri Kigwangalla, Agosti 7 mwaka jana, alitangaza kuiondoa kampuni hiyo katika kitalu hicho, ambacho kimekuwa na  migogoro baina ya kampuni hiyo na vijiji 23 vinavyozungika kitalu hicho, halmashauri na serikali wilaya ya Longido na mkoa Arusha .

Posted by MROKI On Sunday, January 19, 2020 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo