Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2019

Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mradi wa ufugaji nyuki kwenye kilele cha Siku ya Chakula Dunia ambapo siku hii huadhimiswa Kimataifa kila tarehe 16 Octoba ya kila mwaka.
 Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo akitembelea mabanda ya washiriki.
  Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo akitembelea mabanda ya washiriki.
WANANCHI watakiwa kuchangamkia fursa ya ufugaji nyuki iliyoletwa kwao kupitia mradi wa ufugaji nyuki katika kituo cha Kilimo cha Malolo kilichopo Mabwepande Wilayani Kinondoni.

Hayo yalisemwa jana na Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akizindua mradi huo kwenye kilele cha Siku ya Chakula Dunia ambapo siku hii huadhimiswa Kimataifa kila tarehe 16 Octoba ya kila mwaka.

"Niwahimize wananchi waliopo kwenye maeneo ambapo mradi huu utatekelezwa hususani vijana kuchangamkia fursa hii adimu ya kujihakikishia kipato halali kupitia ufugaji nyuki. Kwa kufanya hivyo mtachangia katika utekelezaji wa kauli mbio ya Siku ya Leo inayosema "lishe Bora kwa ulimwengu usio na njaa kufikia 2030", alisema Prof. Silayo.

Aidha, kamishna Prof. Silayo aliwahimiza wakulima, wafugaji, wasindikaji na wadau wengine katika sekta hizo kufanya kilimo chenye tija kwa kuzingatia matumizi sahihi ya technolojia na sheria zinazosimamia uendelezaji kilimo mjini. Prof. Silayo alisema kwa kufanya hivyo itasaidia kubadiri fikra zilizojijenga miongoni mwa wadau mbalimbali kwamba Dar es Salaam haina mazingira salama kwa ajili ya kilimo.
Posted by MROKI On Thursday, October 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo