Mbunge wa Jimbo
la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameomba Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuongeza
kasi ya uboreshaji miundombinu ya barabara jimboni humo ili kuvutia wawekezaji
zaidi.
Biteko
ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ombi hilo Oktoba 15, 2019 kwenye kikao
cha Bodi ya Barabara Mkoa Geita ambacho pamoja na mambo mengine kimejadili utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya barabara.
Amesema wakati
Serikali inaendelea kuboresha mapori yaliyopo wilayani Bukombe kuwa na hadhi ya
kuvutia watalii, ubora wa miundombinu ya barabara utavutia zaidi wawekezaji
hivyo mamlaka hizo ni vyema zikatekeleza miundombinu iliyokwisha ingiza kwenye
mpango.
Naye
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
ameshauri mamlaka hizo ikiwemo TARURA kuzingatia vipaumbele vya wawakilishi wa
wananchi wakiwemo wabunge zinapokuwa zinatekeleza miradi ya barabara.Anaandika George Binagi- BMG
Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko (aliyesimama) ambaye pia ni Waziri wa Madini akizungumza kwenye kikao hicho. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Alhaji Said Kalidushi, Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Mbunge wa Nyang'hwale Nassor Amar pamoja na Mbunge wa Busanda Lolensia Bukwimba.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Busonzo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukombe, Safari Mayala (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko (kulia) ambaye pia ni Waziri wa Madini akikagua taarifa ya utekelezaji miradi mbalimbali ya barabara mkoani Geita. Kushoto ni Mbunge wa Nyang'hwale Nassor.
Tazama Video hapa chini
0 comments:
Post a Comment