Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2019

Mwandishi wetu,Babati.
Miradi yenye thamani ya zaidi ya sh 100 milioni imetekelezwa katika kijiji cha vilima vitatu ,wilayani Babati mkoa wa Manyara kutokana na mchango wa sekta ya Utalii.

Kijiji hicho,ambacho kipo katika eneo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori wa Burunge,kimenufaika na misaada toka mwekezaji kampuni ya Chemchem ambayo imewekeza katika Utalii wa picha na hoteli.

Mwenyekiti wa kijiji hicho,Elasto Balela na Afisa mtendaji wa serikali ya kijiji hicho,Husna Shaban wamesema misaada ambayo wameipata imesaidia sekta ya elimu,afya,ajira na mikopo ya kwa vikundi vya wajasiriamali.

Balela amesema mwekezaji huyo, amesaidia ukarabati na ujenzi shule ya msingi vilima vitatu na shule ya msingi Mdori kwa kutumia zaidi ya milioni 60.

"Mwekezaji amekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo  ya jamii ya vilima vitatu" amesema

Akizungumzia migogoro katika kijiji hicho,alisema aihusiani na mwekezaji bali ni maamuzi ya serikali katika kuhakikisha eneo la uhifadhi na Utalii linalindwa kutoharibiwa.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho,Shaban amesema mwaka 2019 tasisi hiyo pia imetoa fedha kwa vikundi vitano vya akina mama kwa ajili ya ujasiliamali.

"Pia licha ya misaada yote wametoa busi kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa secondarinambao walikuwa wakitembea zaidi ya kilomita 10 kwenda shule" alisema.

Mwenyekiti wa chama cha wavuvi vilima vitatu,Patrick Wambura alisema mahusiano yaliyopo sasa baina yao na wawekezaji yamesaidia uvuvi kufanyika vizuri.

Afisa Maendeleo  ya jamii wa Chemchem,Walter Pallangyo amesema licha ya misaada hiyo mwaka huu,wametoa madawati 100 kwa shule za msingi na sekondari.

Pallango pia amesema wanaendelea na mpango wa kuwasomesha wanafunzi kutoka kaya Masikini katika vijiji 10 vilivyounda jumuiya hiyo.

"Tunawasomesha chuo cha wanyamapori mweka wengine vyuo vya ufundi ili kuweza kubadili maisha yao" alisema

Jumuiya ya uhifadhi ya Burunge kwa sasa ni ya pili nchini kati ya jumuiya 28 kutokana na kuingiza mapato mengi na mwaka 2018/19 wamepata 1.2 billion.
Posted by MROKI On Friday, August 30, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo