Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha maji – Mkwawa, Ahmed Huwel  baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji-Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kuhusu ujazaji maji katika chupa wakati alipozindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maji – Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kutembelea kiwanda baada ya Waziri Mkuu kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji- Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel (wa tatu kulia) kutembelea mitambo ya kuzalisha maji baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa  wa Iringa, Ally Happy na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji- Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
WAZIRI  Mkuu alizindua kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa na kusema kuwa ujenzi huo ni njia ya uhakika ya kupunguza tatizo la ajira na kwamba itaendelea kushawishi wawekezaji wa ndani na nje ili wananchi wengi wapate ajira.

“Serikali imetoa wito kwa wawekezaji wawekeze katika viwanda mbalimbali nchini, hivyo ni muhimu wawekezaji hao wakalindwa na wasibugudhiwe ili waweze kuendelea na uzalishaji wa bidhaa zao. Watumishi mlioajiriwa fanyeni kazi kwa uaminifu.”

Naye,Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha Maji cha Mkwawa,Ahmed Huwel alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kuzalisha na kufanya biashara ya maji safi na salama pamoja na kuunga mkono mkakati wa Serikali wa ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Alisema kiwanda chao kimeajiri watumishi158 kati yao wanaotoka nje ya nchi ni watatu tu na kwa upande wa ajira zisizo rasmi ni zaidi ya 3,000 na kwamba wanatarajia kuongeza ajira kwa wananchi wengi zaidi baada ya kukamilisha ujenzi wa kiwanda kingine cha kutengeneza vinywaji baridi.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazokikabili kiwanda hicho alisema ni pamoja na ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa baadhi ya mitambo hivyo ameiomba Serikali iwasaidie.
Posted by MROKI On Wednesday, September 25, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo