Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2019

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia) wakitazama maziwa yaliyofungashwa wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjni Iringa, Septemba 25, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Septemba 25, 2019.  Kushoto ni Mkugenzi Mtendaji wa Makampni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda hicho, Fuad Abri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  wakitazama mitambo ya kusindika maziwa na bidhaa zake   wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri,  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Fuad Abri na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Balozi wa bidhaa za maziwa za ASAS na Msanii maarufu nchini, Mai Zumo wakati walipotemblea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
 ****************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kudhibiti uingizwaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 25, 2019) alipotembelea kiwanda cha maziwa cha Asas, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia sekta ya viwanda.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi.

“Serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya mifugo ili kuhakikisha inaleta tija kwa wafugaji na taifa kwa ujumla, hivyo wafugaji endeleeni kuimarisha ushirika wenu. Wizara ya Mifugo iendelee kuwaelimisha wafugaji ili wafuge kitaalamu.”

Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya Asas kwa sababu ni miongoni mwa kampuni chache ambayo imeanza kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna bora ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni bora za ufugaji wa kisasa pamoja na kuwapa uhakika wa soko.

Amesema Serikali inathamini sana uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Asas kwa sababu wameitikia wito wa Serikali wa ujenzi wa uchumi kupitia sekta ya viwanda, hivyo itahakikisha wawekezaji wote wananufaika na uwekezaji wao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Maziwa cha Asas, Fuad Abri amesema kiwanda chao kinampango wa kupanua uzalishaji kwa kujenga kiwanda kingine cha kusindika maziwa katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na kipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Posted by MROKI On Wednesday, September 25, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo