Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imefanikiwa kutoa Mikopo ya Asilimia 10 kama takwa la kisheria na maelekezo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Mwinyi Omary Mwinyi amesema jumla ya Kiasi cha Shilingi Milioni 177 zimetolewa kwa vikundi hivyo tarehe 06/02/2025 ikiwa ni awamu ya kwanza ya kutoa mikopo.
Aidha Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa awamu ya pili imeanza kwa usaili wa vikundi mbalimbali kuanzia tarehe 02-30/02/2025 ambapo jumla ya shilingi milioni 500 zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vitakavyopitishwa.
0 comments:
Post a Comment