Nafasi Ya Matangazo

August 17, 2019

Afisa wa Fedha wa MISA-Tanzania, Glory Mwakalinga akizungumza katika kongamano hilo.
Watoa mada katika kongamano hilo 
Mwanahabari Mwandamizi,Mussa Juma, Akitoa mada juu ya usalama kwa wanahabari na uhalifu wa mitandao, na kusema ni muhimu katika utendaji kazi wanahabari kuzingatia tahadhali za kiusalama na matumizi sahihi ya mitandaoya kijamii.
Mwezeshaji mhariri wa siasa katika gazeti la mwananchi,Tausi Mbowe aliwataka wanahabari katika utendaji wa kazi zao, kuzingatia sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.
***********
Mwandishi wetu,Singida. 
Waandishi wa habari nchini,wametakiwa  kujilinda na uhalifu wa mitandao  kuwa na  tahadhari za kiusalama katika utendaji kazi.

Wito huo, umetolewa  katika mjadala wa siku moja wa wanahabari mkoani Singida, ambao uliandaliwa na taasisi MISA Tanzania, kwa udhamini ya taasisi ya Internews kupitia mradi wa Boresha Habari, shirika la msaada la Marekani(USAID) na taasisi ya  fhi360.

Akitoa mada juu ya usalama kwa wanahabari na uhalifu wa mitandao, mwanahabari Mwandamizi, Mussa Juma amesema ni muhimu katika utendaji kazi wanahabari kuzingatia tahadhali za kiusalama na matumizi sahihi ya mitandaoya kijamii.

Juma amesema wanahabari wanapaswa kuijua sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 na Kanuni   za sheria ya mawasiliano ya kielekroniki na Posta ya mwaka 2018.

"lakini pia kutokana na mazingira ya sasa ya kazi ya uandishi ni muhimu kufanyakazi ya kuzingatia usalama ikiwepo kuwa na mpango kazi wa kila siku na kufanya tathimini ya madhara ambayo yanaweza kutokea"alisema

Akizungumza katika mjadaa huo, kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Atubone Mwakalekwa, alishukuru MISA kuandaa mjadala huo kwani  ni mara  ya kwanza kuwakutanisha wanahabari na wadau wa habari.

Alisema Jeshi la polisi,mkoa wa Singida linajitahidi kuboresha mahusiano baina ya wanahabari na polisi  na kutaka uwepo ushirikiano katika utendaji wa kazi.

Mwezeshaji mhariri wa siasa katika gazeti la mwananchi,Tausi Mbowe aliwataka wanahabari katika utendaji wa kazi zao, kuzingatia sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.

"Kazi ya uandishi wa habari kwa sasa inahitaji weledi mkubwa ikiwemo kujua sheria kwani kutojua sheria mbali mbali sio utetezi"alisema

Mjadala huo,ulihusisha wanahabari mkoani Singida, maafisa habari wa halmashauri, jeshi la polisi na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Singida.
Posted by MROKI On Saturday, August 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo