Nafasi Ya Matangazo

August 17, 2019


Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha kisusa kilichopo katika kijiji cha Ukami wakati akiwaeleza lengo la kujenga kituo cha afya cha kata ya Mapanda.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo katika kijiji cha Ukami wakati akiwaeleza lengo la kujenga kituo cha afya cha kata ya Mapanda
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Mapanda wakati akiwaeleza lengo la kujenga kituo cha afya cha kata ya Mapanda

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Chogo wakati akiwaeleza lengo la kujenga kituo cha afya cha kata ya Mapanda


Na Fredy Mgunda, Iringa
ZIARA ya Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini imeanza kuzaa matunda baada ya kuamua kuanza kujenga kituo cha afya cha kata ya Mapanda ambacho kitakuwa msaada mkubwa katika kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara ya vijiji vya  Mapanda,Chogo,Ukami,Uhafiwa, Ihimbo pamoja na vitongoji vya Mtwivila na Kisusa mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa alisema kuwa imefika wakati wa kuhakikisha wanapata kituo cha afya ili kuboresha huduma za afya katika kata hiyo.

“Mtake mistake kituo cha afya kitajengwa hapa kwa mchango wangu kama mbunge,mchango wa serikali pamoja na nguvu zenu wananchi kwa pamoja tutaweza kufanikisha swala hili na mimi kama mbunge sipo tayari kuona kituo hiki hakijengwi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wakianza ujenzi wa kituo hiki cha afya cha kata atachangia mifuko mia mbili ya saruji kwa awamu hiyo ya kwanza kama kuwaunga mkono ila ataendelea kuchangia katika ujenzi wa kituo hicho cha afya.

“Mimi nimeanza kwa kuchangia mifuko hiyo ya saruji ila nitawatafuta wadau wengine kuhakikisha wanatuchangia ili kupunguza mzigo wa michango kwenu wananchi ambao ndio mmeniweka madarakani hadi hii leo” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa atahakikisha wawekezaji wote ambao wanaizunguka kata ya Mapanda wanachangia shughuli za maendeleo kwa kuwa wamekuwa wakitajilika kutumia ardhi iliyopo katika kata hiyo.

Aidha Mgimwa alisema kuwa wakianza ujenzi wa kituo hicho cha afya atahakikisha waziri wa TAMISEMI Salemani Jafo anafika katika eneo la ujenzi na kutoa mchango wa serikali kwa kuwa serikali huwa inachangia pale ambapo wananchi wameanza kufanya maendeleo.

“Waziri Jafo lazima atakuja tu kufanya mkutano wa hadhara hapa katika eneo hili ambalo kituo cha afya kitajengwa hicho wananchi lazima muanze ujenzi wa kituo hiki” alisema Mgimwa

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mikutano hiyo walisema kuwa wapo tayari kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha afya ili kuboresha sekta afya ambapo wamekuwa wakiteseka kwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Posted by MROKI On Saturday, August 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo