Nafasi Ya Matangazo

August 25, 2019

DStv Tanzania imethibitisha rasmi kupunguza kwa kiasi kikubwa ada ya mwezi ya vifurushi vyake kuanzia Septemba mosi, 2019.

Mabadiliko hayo yanakuja muda mfupi tu baada ya kuanza kwa msimu wa soka ambapo ligi kubwa maarufu diniani zimeanza hivyo kuwawezesha wateja wa DStv kushuhudia ligi hizo kwa bei nafuu sana.

Akithibisha punguzo hilo la bei, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema kuwa muda wote wamekuwa wakisikiliza maoni ya wateja wao na moja ya mambo wateja waliyoshauri ni kupunguzwa kwa bei za vifurushi. 

"Wateja ndiyo moyo wa biashara yetu na muda wote tunawasikiliza na kutekeleza maoni yao pale inapowezekana. Kwa msingi huu, tumeamua kupunguza bei ili wateja wetu waendelee kufurahia burudani kabambe kwa bei nafuu zaidi“ alisema Jacqueline.

Amezitaja bei hizo mpya kuwa kifurushi cha DStv Premium kutakuwa na punguzo la Sh 40,000 kutoka bei ya sasa ya Sh 169,000 hadi 129,000; Kifurushi cha DStv Compact+ punguzo la Sh 25,000 kutoka 109,000 hadi 84,000;  Kifurushi cha DStv Compact punguzo la Sh 25,000 kutoka 69,000 hadi  44,000; na kifurushi cha DStv Family punguzo la Sh 10,000 kutoka 39,000 hadi 29,000.

Kuhusu vifurushi maalum, Jacqueline amesema kifurushi chenye nyongeza maalum ya chaneli za Asia - DStv Premium+Asia Addon kitapungua kwa shilingi 40,000 kutoka 220,050 hadi 170,050 wakati kile chenye chaneli za ziada za Kifaransa DStv Premium+French addon nacho pia kitapungua kwa 40,000 kutoka 259,000 hadi 2019,000. 

Mkurugenzi huyo amewahakikishia wateja wa DStv kuwa kushuka huko kwa bei hakutasababisha mabadiliko wa chaneli katika vifurushi hivyo mteja ataendelea kupata chaneli zile zile alizokuwa akipata awali ila sasa atakuwa analipa bei ndogo zaidi.

Posted by MROKI On Sunday, August 25, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo