Nafasi Ya Matangazo

August 26, 2019

Nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor akinyanyua kombe juu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Charteredb Bank Ajmair Riaz mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa TFF Bw. Wallace Karia kushoto kwenye michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019
Rais wa TFF Wallace Karia akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank Ajmair Riaz.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Charteredb Bank Ajmair Riaz akinyanyua kombe na nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor mara baada ya kukabidhiwa.
Wachezaji wa timu ya wa timu ya Dar es Salaam Corridor mara baada ya kukabidhiwa nishani zao kabla ya kukabidhiwa kombe.
Wachezaji wa timu ya wa timu ya Dar es Salaam Corridor wakiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI

Timu ya Coca Cola jezi nyekundu ikichuana na timu ya Dar es Salaam Corridor katika michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki hiyo, Juanita Mramba akizungumza na wanahabari kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019 kuhusu michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 .
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akijadilia jambo na waratibu wa michuano hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019.
Timu ya Coca Cola na Airtel zikichuana kwenye pambanpo la awali la fainali hizo.Coca Cola ilishinda mabao 2-0.
Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na Ali Mayayi Mchezaji wa Zamani na Mchambuzi wa soka katika fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019.
Baadhi ya watu waliohudhuria katika michuano hiyo kutoka makampuni mbalimbali ambao ni wateja wa benki ya Tandard Chatered jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakizungumza na baadhi ya waratibu wa michuano hiyo.
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akizungumza jambo na MC wa michuano hiyo.
Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakikagua timu ya Dar es salaam Coridor kabla ya fainali za michuzno hiyo.
Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Bw. Wallace Karia na wadau wengine.
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Dar es salaam Coridor.
****************
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz amesema kombe la Standard Chartered ni michuano inayokwenda sambamba na ushirikiano wao na timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) Liverpool ambapo benki hiyo imekuwa ni mfadhili wa timu hii tangu mwaka 2010.

Ajmair Riaz amesema wamekuwa wakifanya miradi mbalimbali ya michezo wakishirikiana na timu ya Liverpool, na kombe la Standard Chartered ni mojawapo ya michuano ambayo imekuwa ikifanyika katika nchi mbalimbali ambapo biashara ya benki hiyo ipo katika mabara ya Asia, Africa na Mashariki ya Kati.

Bw. Ajmair Riaz ameyasema hayo wakati wa fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya Agosti 24, 2019.

"Wengi wenu mtakumbuka michuano ya mwaka juzi, 2017, ambapo timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders iliibuka na ushindi na kwenda kwenye mashindano ya fainali pale Anfield Uingereza ambako pia walicheza vizuri na kuiinua bendera ya Tanzania vyema! Hii ilikuwa ni baada ya kuzishinda timu washindi za Kenya na Uganda katika michuano ya mabingwa wa Afrika Mashariki" Amesema Ajmay Riaz.

Amesema mwaka jana walitangaza mfumo mpya wa michuano hii ambapo walianzisha mashindano ya kitaifa tu. Mfumo huu hauhusishi tena mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki ya kuwania safari ya kwenda Anfield Uingereza kwa kupambana na washindi wa nchi za Kenya na Uganda!

Ameongeza kuwa mwaka huu wanaendelea na mfumo huu na timu itakayoshinda michuano hii ya kitaifa, , itakuwa imejishindia safari ya kwenda Anfield Uingereza moja kwa moja! badala ya kuchuana na nchi za Afrika Mashariki tena.

Alitangaza kuwa timu ambayo itaibuka kuwa mshindi katika mashindano hiyo moja kwa moja itakwenda nchini Uingereza, Anfield, kuangalia mchezo mkali wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu ya Liverpool na timu ya Watford, utakaofanyika tarehe 14 Disemba mwaka huu.

"Benki ya Standard Chartered itagharamia safari za wachezaji saba wa timu hiyo, yaani tiketi za ndege, na malazi yao kwa siku tatu. Pia wakiwa kule Uingereza watakuwa na ratiba nzuri kabisa itakayohusisha matembezi katika uwanja wa Anfield, na pia watakutana na magwiji mbalimbali wa timu ya Liverpool.

"Ninafurahi kuwajulisha kuwa tiketi za mechi hii kwa ajili ya washindi wetu wa siku ya leo tayari zimeshaandaliwa" alisema, Ajmay Riaz.
Aliwashukuruwageni waliofika katika viwanja vya JK Park kwa ajili ya michuano hiyo na washiriki wote wa awamu ya nne ya michuano ya kombe la Standard Chartered ambapo historia nyingine itawekwa .
Posted by MROKI On Monday, August 26, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo