Na mwandishi wetu,Arusha
Taasisi za Chemchem Association imepanga kutumia zaidi ya sh 100 milioni mwaka mwaka 2019 kuchangia miradi ya Maendeleo katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Wanyamapori( JUHIBU) .
JUHIBU, ilianzishwa mwaka 2003 inaundwa na vijiji vya Sangawe, Mwada,Ngoley, Vilimavitatu, Minjingu,K Olasiti,M Magala, na Maweni na ina ukubwa wa 283.
Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, Walter Palangyo alisema taasisi inachangia miradi hiyo kama sehemu ya wajibu wake kuchagia shughuli za Maendeleo ya jamii(SCR) mbali ya kodi na tozo nyingine zinazolipwa na Chemchem iliyowekeza shughuli za Utalii katika hifadhi hii.
Alisema taasisi hiyo, imekamilisha ukarabati wa majengo ya shule ya msingi vilima vitatu,ofisi mbili za walimu na sasa mradi wa ujenzi wa vyoo .
"katika shule hii, tumetumia kiasi cha sh 50 milioni, ili kuhakikisha wanafunzi katika shule hii wanapata elimu bora katika mazingira mazuri kwani tayari tumewapatia madawati 100 kwa ili kumaliza tatizo katika shule hii"alisema
Alisema taasisi hiyo pia imetoa kiasi cha sh 5 milioni ili kusaidia Vikoba katika baadhi ya vijiji katika eneo hilo, ikiwepo vikundi vya jamii ya wabarbeig ili kuweza kuwa na miradi ya maendeleo.
"kuna kikundi cha Wicheda na Datoga vya jamii ya kibarbeig ambavyo tumepatia kiasi cha sh 2.5 milioni ili kukuza mitaji yao"alisema
Alisema katika jamii hiyo, pia kumeanzishwa mradi wa maboma ya asili ambayo watalii wataweza kuwatembelea .
"Mwaka huu pia tunaendelea na mradi wa kusomesha watoto katika jamii hii, katika chuo cha wanyamapori cha Mweka na chuo cha Ufundi (VETA) naa wengine tumewalipia ada za shule ya sekondari "alisema
Alisema pia kuna miradi ya maji, michezo na afya katika vijiji hivyo, hasa kutokana na fedha ambazo zinatokana na la ya utalii.
0 comments:
Post a Comment