SHIRIKA la Maendeleo ya Mafuta
Tanzania (TPDC), limempa tuzo Waziri wa
zamani wa Serikali ya Tanzania, Prof Mark Mwandosya kutokana na mchango wake
mkubwa katika maendeleo ya shirika hilo.
Mwandosya amepata kuhudumu
TPDC kwa nafasi ya Kamishna wa kwanza wa
Petroli nchini na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika hilo.
Tuzo hiyo ilitolewa wakati
shiruka hilo likiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri Mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, ambaye aliwakilishwa na Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuuu- Uwekezaji Mh. Angela Jasmine
Kairuki.
TPDC ilitumia maadhimisho hayo kutoa TUZO kwa baadhi ya Wawstaafu waliokuwa na
michango mbalimbali katika utumishi wao.
Pichani (juu) ni Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemuakimkabidhi tuzo Prof Mwandosya kwa
niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TPDC
0 comments:
Post a Comment