Nafasi Ya Matangazo

June 17, 2019

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kufanya kikao na wakurugenzi wa taasisi 16 na bodi zilizochini ya wizara hiyo, jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya ushindani Hamfrey Mosha, akizungumza na wanahabari mda mfupi baada ya kufanya kikao na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini Dodoma.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usajili wa biashara na leseni, Emanuel Kakwesi, akizungumza na wanahabari mda mfupi baada ya kikao cha wakuu wa taasisi na bodi zilizochini ya Wizara hiyo na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini Dodoma.

Picha na mpiga picha wetu.

                           ********

Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.

WAZIRI wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amezitaka taasisi zilizochini ya wizara hiyo kutengeneza mipango wezeshi ambayo ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na kutufikisha katika uchumi wa viwanda, mipango ambayo haitakuwa kandamizi kwa wawekezaji.

Sambamba na kujenga uhusiano mzuri baina ya taasisi hizo na wenye viwanda, wafanya biashara ili kwa pamoja kuona changamoto ambazo zinawakabiri wafanyabiashara ambazo ni kikwazo kufikia malengo.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi baina ya wakuu wa taasisi kumi na sita (16) pamoja na bodi zilizochini ya wizara hiyo, waliokutana kwa siku mbili Dodoma kujadili mbalimbali na namna ya kufikia walengo ya serikali.

Amezitaka taasisi hizo kuja na mbinu ambazo zitasaidia kuinua sekta hiyo bila kuathiri wawekezaji na kukaa na wawekezaji kubaini changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao.

“Lengo la kikao hiki ni kukaa na taasisi zetu ili kuona namna bora ya kufikia malengo tuliyojiwekea na mambo ambayo ni kikwazo katika kutekeleza, sasa niwatake taasisi msiwe kikwazo kwa wawekezaji, mtengeneze mipango ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na mipango ambayo haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji” amesema Bashungwa.

Ametolea mfano kwa shirika la viwanda Tanzania TBS kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa kuwa na viwango, pia katika kudhibiti viwango wahakikishe hawaathiri wala kuchelewesha shughuri za mwekezaji.

Amesema katika kikao ambacho Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alikaa na wafanyabiashara ikulu kilimpa mwanga namna ya kuja kufanya kazi ndani ya wizara hiyo na atahakikisha anasimamia kikamilifu wizara hiyo.

Amesema matokeo ya kikao hicho tayari yameanza kuonekana ambapo kodi na tozo zilizokuwa kero zimeondolewa zaidi ya 54, amesema sambamba na hilo atahakikisha anafanya mageuzi katika sekta hiyo.

Kwa sababu amebaini kuwa unaweza kufuta kodi hizo lakini tatizo likabaki palepale, amesisitiza kwenye taasisi kuimarisha mahusiano na wawekezaji na namna ya kuongea na wafanyabiashara, linaweza kuwa sida sio kero ya kodi bali ni mahusiano baina yao.

Amebainisha kuwa kuna haja ya kufungamanisha sekta ya kilimo na viwanda ili kuleta matokeo chanya katika wizara ya viwanda na biashara, amesema kuna uhusiano mkubwa baina ya kilimo na viwanda hivyo vikifungamanishwa vinaweza leta matokeo mazuri.

Amesema ataimarisha mahusiano na jumuiya ambazo Tanzania ni mwana chama kama EAC na SADC ili tuweze kufaidika na kuwa wanachama kwa sababu Tanzania inalipa ada kila mwaka ni lazima ione matokeo yake na hasa katika sekta ya uwekezaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya tume ya ushindani Hamfrey Mosha, amesema kikao hicho kilikuwa na faida kwa sababu kimezikutanisha taasisi kumi na sita(16) zilizochini ya wizara hiyo na kujiona kumbe wanaweza kufanya jambo ila walikosa nafasi tu kama hiyo.

“Kikao kimekuwa kizuri taasisi zaidi ya 16 tumekutana jambo ambalo halijawahi kufanyika na kwa kikao hiki tumejiona kumbe tunaweza kufanya jambo ndani ya wizara hii” amesema.

Amesema wao kama tume ya ushindani wanafanya kazi kwa weredi mkubwa kwa kudhibiti bidhaa bandia kuingia nchini kwa kuhakikisha tunakagua makontena yote yanayoingia katika bandari zetu.

Posted by MROKI On Monday, June 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo