Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2019


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akieleza jinsi gani atakavyo hakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa wanaojenga hospitali hiyo ili kusitokee kasoro zozote zile.
 Haya ni baadhi ya majengo yaliyojengwa katika hospitali ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa ambayoWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa unaotekelezwa kwa kutumia  zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukagua hospitali hiyo Waziri Jafo amesema kuwa kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo inaridhisha na baada ya kukamilika kwake itawasaidia wananchi wengi wa maeneo hayo pamoja na kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa.

“Niwahakikishieni viongozi wa wilaya na mkoa kuwa nimeridhishwa na kasi hii ya ujenzi wa hospitali hii kwa kuwa mnasimamia vilivyo kwa kuhakikisha fedha za serikali zinatumia vizuri hivyo niwapongeze sana” alisema Jafo

Jafo alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo makini katika kuhakikisha wananchi wa chini wanapata huduma muhimu bila kizifuata kama ilivyokuwa awali na amehaidi kuwa atazifukisha salamu kwa Mheshimiwa Rais juu ya hatua ambazo zinaendelea katika hospitali hiyo

“Leo naweza kuwapongeza mmefanya kazi kubwa ya kusimamia ujenzi huu ambao umekuwa ukienda vizuri kila hatua ambayo nimekuwa nikifuatia hatua kwa hatua hadi hii leo naona matunda yake” alisema Jafo

Aidha Jafo aliwataka viongozi kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa majengo hayo kumalizia vizuri ili kuondokana na kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zimejitokeza hasa kwenye milando bado kunashida kuhatajikajia kurekebishwa.

“Nimetembea kwenye majengo haya yamejengwa vizuri kwa kufuata vigezo stahili lakini tatizo ambalo nimelibaini ni kuwa mirango haijakaa vizuri inahitajika kutolewa na kuwekwa milango mipya hivyoa naombeni hakikisheni mnasimamia” alisema Jafo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema kuwa wataendelea kuwasimamia wakandarasi hao ili kuhakikisha wanarekebisha kasoro zote ambazo zimejitokeza katika hatua hizo za umaliziaje wa ujenzi huo wa hospitali hiyo ya wilaya ya Kilolo.

“Mheshimiwa waziri tumezipokea pokea kasoro hizo ambazo umetuagiza tumsimamie waha wakandarasi na sisi tutazisimamia vilivyo ili kupata hospitali iliyo bora kwa kila kitu na kuwa mfano wa kuigwa kwa hospitali nyingine” alisema Hapi

Hapi alimuomba waziri Jafo kuhakikisha anawafikishia shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kwa kuwapa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya mkoa wa Iringa.

“Kwa kweli tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kuendelea kutuletea fedha kwenye miradi mingi ya kimkakati hivyo tunashukuru sana” alisema Hapi

Naye mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa atahakikisha kila uchwao anaendelea kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuwa ipo katika wilaya yake.

“Mimi nitaendelea kusimamia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyokusudiwa na kuwa hospitali ya mfano hata nchini hivyo nikuahidi nimeyachukua kwa umakini mkuwbwa maagizo yako” alisema Abdalah
Posted by MROKI On Monday, May 20, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo