Nafasi Ya Matangazo

May 19, 2019

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Vuo wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, kabla ya kuwasha umeme kijijini hapo akiwa katika ziara ya kazi Mei 18, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), alipokuwa katika ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Mei 18, 2019
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme vijijini mkoani Tanga, Ahmed Hemed kutoka kampuni ya JV RADI Services Njarita & Aguila (kushoto), akizungumza na wamiliki wa nyumba inayoonekana pichani, Sabasaba Hassan na mama yake, muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuiwashia umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Mei 18, 2019.

 Na Veronica Simba - Tanga
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, ameuagiza uongozi wa juu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukata asilimia 10 ya malipo ya Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga, endapo itabainika hana sababu za msingi kuchelewesha mradi.

Alitoa maagizo hayo Mei 18 mwaka huu katika Kijiji cha Vuo, Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

Akizungumza na wananchi wa Vuo, kabla ya kuwawashia rasmi umeme, Dkt. Kalemani alisema kasi ya mkandarasi hairidhishi maana ni ndogo sana hivyo akawataka watendaji wa TANESCO kufuatilia ili kujiridhisha endapo kuna sababu za msingi za ucheleweshaji huo wa mradi.

"Mkurugenzi TANESCO fuatilia; ukikuta kuna uzembe, wakate asilimia 10 ya mshahara wao maana wanataka kutucheleweshea mradi."

Sambamba na agizo hilo, Waziri alielekeza mkandarasi huyo kuwa na Mpango-Kazi wenye mchanganuo wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki.

Kufuatia agizo hilo, alimtaka Meneja wa TANESCO wa Wilaya, kumwandikia barua ya kusitisha mkataba wake, Mkandarasi husika endapo atashindwa kuwasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki.

Aidha, Waziri alimtaka Meneja huyo pamoja na Mkandarasi kuwasilisha maelezo ndani ya siku moja sababu za kusuasua kwa utekelezaji wa mradi.

“Meneja wewe ndiye wa kumsimamia Mkandarasi. Kama kasi yake ni duni, inamaanisha hata wewe utendaji wako siyo mzuri,” alisema Waziri.
Posted by MROKI On Sunday, May 19, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo