Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2019

Mwanamuziki nguli raia wa Zimbabwe, Oliver "Tuku" Mtukudzi amefariki dunia hii leo.

Mtukudzi amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Avenue jijini Harare akiwa katika wodi ya Wagonjwa walio katika uangalizi maalum (ICU).

Mtukudzi alizaliwa Septemba 22, 1952 mjini Highfield, Harare na amefikwa na umauti akiwa na miaka 67 . 

Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Thomas Mapfumo.

Nyimbo ya kwanza ilikuwa "Dzandimomotera" iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. 

Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki. Anafurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. 

Oliver ametoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata zingine hawezi kuzikumbuka.
Posted by MROKI On Wednesday, January 23, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo