Nafasi Ya Matangazo

December 14, 2018

Hatimaye kipindi maarufu cha Shilawadu kuanza kuonekana live ndani ya DStv kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo (DSTV160) kuanzia Ijumaa Desemba 14, 2018. Shilawadu Xtra itaruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja jioni na kurudiwa siku za Jumapili muda huo huo.

Akitambulisha rasmi wa kipindi hicho, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwa kipindi cha Shilawadu Xtra kimeongezwa ladha kadha wa kadha tofauti na awali  na kitagawanyika katika sehemu tofauti tofauti ikiwamo Chemba la Msengenyo, Ubuyu wenye Vitamin Xtra, Kiti cha Moto na Mikikimikiki ya mastaa  ili kuwapatia wateja wa DStv na watazamaji kwa ujumla burudani isiyo kifani .                                            asfgd_00000
Amesema kuwa watazamaji wa Maisha Magic Bongo na wapenzi wa Shilawadu hasa wale wapenzi wa umbea wakae mkao wa kula kwani kwa sasa wataweza kushuhudia visa na matukio yote yanayojiri hapa mjini kupitia Shilawadu Xtra chini ya makamanda mahiri wa kipindi hicho akiwemo mkali wa kunyapianyapia Soudy Brown sambamba na kamanda Kwisa ‘Mzee mti mkavu’.

“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic Bongo(MMB), siku zote tunafanya jitihada kuhakikisha kuwa tunatoa kipaumbele na kuunga mkono maudhui ya ndani na kipindi hiki ni muendelezo wa jitihada hizo”, alisema Alpha.

Kipindi hiki kitakuwa kikiruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja hadi saa mbili usiku na kurudiwa kila Jumapili kwa muda huo huo. Hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi na haswa kwa wale ambao hawataweza kukitazama kwa siku ya Ijumaa.
Posted by MROKI On Friday, December 14, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo